0
MSHAMBULIAJI WA SIMBA EMANUELI OKWI
Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi anatarajiwa kwea pipa na kuondoka nchini kuelekea Denmark katika klabu ya Sonderjyske iliyopo kwenye Danish ligi ya Superliga kwa majaribio.
Majaribio hayo yatakuwa ya siku 14 kuanzia tarehe 08/07/2015 na baada ya hapo klabu hiyo ya Sonderjyske itatuma ripoti kamili ya majaribio yake.
Tovuti ya Simba Rais wa klabu, Evans Aveva amesema Simba inafurahi sana kuona wachezaji wake wanapata nafasi hizi za kuonesha vipaji vyao tena kwenye viwango vya kimataifa zaidi.
“Simba inamtakia kila la kheri Okwi kwenye majaribio yake ya siku 14 kwnye klabu ya Sonderjyske iliyopo kwenye Danish Superliga”amesema Aveva

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top