0
mshambuliaji wa azam John Boko (adebayor)
Klabu ya Free State Stars ya Afrika kusini imenasa saini ya mshambuliaji wa AZAM FC John Bocco ‘Adebayor baada ya klabu yake kukubali kuuza kwa dola 80000 za kimarekani sawa na
milioni 160 za Kitanzania.
Bocco ataungana na Mrisho Khalfan Ngassa aliyesajiliwa na Free State Mei mwaka huu kutoka Yanga SC, ambaye ndiye aliyewapa namba viongozi wa timu hiyo na kuhakikisha Bocco
anatua na kukipiga katika klabu hiyo.
FS imempa mshahara mara mbili ya ule anaopata Azam FC kwa sasa, lakini mchezaji huyo anataka apewe na nyumba pia na baadhi ya vipengele virekebishwe.
Azam FC sasa iko radhi kabisa kumuacha Bocco aende kupata changamoto nyingine baada ya kuitumikia timu kwa zaidi ya miaka saba tangu haijapanda Ligi Kuu.
Awali, Azam FC ilikataa kumuuza Bocco Israel, Afrika Kusini na Algeria licha ya kufuzu majaribio huko- lakini sasa amepata zali la kuchukuliwa bila majaribio.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top