Aliyekuwa Mbunge wa viti maalum kwa
tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Leticia Nyerere
ametangaza kuCihama rasmi chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi
(CCM).
Akizungumza mapema hii leo katika
Mkutano uliofanyika na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara
ya Habari Maelezo jijini Dar, Leticia alisema kuwa, ameamua kurudi CCM
kwani ndicho chama kilichomzaa, kumlea na kumkuza. Leticia ameongeza
kuwa kwa sasa hawezi kuzungumzia kuhusu kugombea tena kiti hicho.
Post a Comment Blogger Facebook