Makamu wa rais wa zamani wa
shirikisho la Soka duniani FIFA Jeffery Webb amekanusha mashtaka ya
ufisadi mbele ya mahakama mjini New York.
Ameachiliwa kwa dhamana
ya dola milioni kumi, kwa sharti kuwa asisafiri umbali wa kilomita
thelathini kutoka mahakama hiyo na mienendo yake yote inachunguzwa kwa
njia ya elektroniki.Bwana Webb alirejeshwa kwa lazima nchini Marekani wiki iliyopita kujibu mashtaka, ambapo anashutumiwa kupokea mamilioni ya dola kama rushwa ili kutoa haki za mauzo na matangazo ya biashara wakati wa mchezo huo.
Yeye ni miongoni mwa maafisa wengine sita wa shirikisho hilo waliokamatwa mjini Zurich mwezi Mei kufuatia uchunguzi wa FBI wa ufisadi ndani ya shirikisho hilo.
Washukiwa hao wengine bado wanapinga kurejeshwa Marekani kwa kesi hiyo.
Post a Comment Blogger Facebook