WANACHAMA Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Kata ya Ruaha, Jimbo la Mikumi, Wilaya ya Kilosa,
Morogoro, wamewavua uongozi waliokuwa viongozi wao na kuweka Kamati ya
Muda (Task Force), kwa madai ya kuwa Mamluki ndani ya chama chao.… (endelea).
Waliovuliwa uongozi na kubaki na uanachama ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kata, George Banda, Katibu wa Chama hicho, Ally Mponda, Katibu Mwenezi, William Temu, Mweka Hazina, Aurelia Mnunga, na Mjumbe wa Kamati Tendaji, Mwalimu Myami.
Katika Kikao cha ndani cha Julai 2
(Ukumbi wa Linas), kilichosimamiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mafunzo
wa Chadema Taifa, Benson Kigaila; Baada ya kusikiliza ‘tuhuma’ za hao,
aliwauliza wanachama wanataka nini, ambapo wote walipaza Sauti; wavuliwe
uongozi na kubaki wanachama!.
Aidha tuhuma zilizoelekezwa kwa Viongozi
hao, ni kuwafukuza viongozi wenzao watatu wa Chadema, kwa kutumia
vifungu visivyokuwemo kwenye Katiba ya Chadema, ilihali wakijua ni
kukinyang’anya Chadema Ushindi wake halali na kukifurahisha Chama
Mapinduzi(CCM).
Tuhuma nyingine zinazowakabili viongozi
hao ni kuhamisha vikao vya Chama, ambapo badala ya kufanyia kwenye Ofisi
ya Chadema Kata, kwa miezi zaidi ya minne walihamishia vikao na Ofisi
kwenye mgahawa wa mmoja wa viongozi hao kinyume cha katiba.
Kiongozi Mpya, Abasi Longa, alikiri
kuchaguliwa Mwenyekiti wa muda kati ya viongozi waliochaguliwa na
wanachama; Hii ikiwa ni mara tu baada ya kumvua, Banda aliyekuwa
Mwenyekiti, ambapo, Joram Zacharia, alithibitisha kuchukua Katibu
aliovuliwa, Mponda.
Mbali ya waliovuliwa nyadhifa kutotaka
kuzungumza na Mwandishi hata walipopigiwa simu za viganjani kuelezea
walivypokea kuvuliwa uongozi na kuwa wananchama; Aliyekuwa
Katibu,Mponda, pekee alikiri kuondolewa, akisema, “Siasa ni kijiti,
lazima tupokezana”.amesema
Hata hivyo, Longa alikiri kupokea fomu za
viongozi watatu waliovuliwa Uongozi na kubaki Wanachama wa Chadema,
Banda, Mponda na Mnunga, ambao wametia nia ya Udiwani wa Kata hiyo.
Awali Mponda, alimthibitisha mwandishi wa
habari, kuhusu azma yake kutia nia ya kugombea udiwani wa Kata hiyo
wakiwemo viongozi wenzake waliovulia madaraka, jambo ambalo limeendelea
kuwawatia shaka wana Chadema kuwa, huenda kulikuwa na kitu nyuma ya
pazia.
Post a Comment Blogger Facebook