ROBERT Kisena ambae ni mmiliki wa Kampuni
ya usafiri Dar es Salaam (UDA), anasakwa baada ya kushindwa kufika
mahakamani kusomewa shitaka la kughushi linalomkabili.… (endelea).
Kusakwa kwa Kisena ambae pia ni mmiliki
wa Kampuni ya Simon Group ni baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
kutoa hati hati ya kumkamata mbali nae wengine ni Ofisa ukaguzi
mwandamizi wa Benki ya TIB, Adam Yusuph na muhasibu wa Simon Group,
Venancy Matondo aliyeunganishwa wanadaiwa kudhamiria kughushi hati ya
malipo kuonyesha kuwa chama cha ushirika cha Shinyanga kilisambaza
mbegu zenye thamani ya Sh. 145 milioni.
Hakimu Thomas Simba alitoa hati hiyo ya kukamatwa kwa wawili hao baada ya mwendesha mashitaka kwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Josheph Kiula kudai kuwa Kisena alifikishiwa wito wa kuitwa mahakamani na akausaini , lakini jana hakutokea mahakamani na hivyo kuomba hati ya kumkamata.
Kiula alidaiwa kuwa, walimpigia simu
mkurugenzi huyo mtendaji wa kampuni ya Simon Group inayomilikiwa na
(UDA) na kumweleza kuhusu wito huo na akawajibu kuwa angefika
mahakamani jana , kitu ambacho hakutekeleza.
Kuhusu mtuhumiwa mwingine, Kiula alidai
kuwa, wito wa kufika mahakamani ulipokewa na kusainiwa na mkewe .Lakini
akasema kuwa Yusuph amekuwa hapatikani kwa simu na kwamba imekuwa
vigumu kumpata ofisini kwa kuwa anahisi anahamahama benki.
Baada ya kutoa maelezo hayo hakimu aliridhia na kutoa hati ya kuwakamata kama ilivyoombwa na wamiliki wa takukuru.
Kiula alidai kuwa, katika kesi hiyo ya
kugushi inawakabili washitakiwa hao, yumo matando ambaye alikuwepo
mahakamani na alisomewa shitaka lake.
Katika shitaka lao, inadaiwa kuwa,
Oktoba 18, 2009 wakiwa jijini Dar es Salaam, watu hao walidhamiria
kughushi hati ya malipo namba 346 ambayo ilikuwa ikionyesha kuwa chama
cha ushirika cha shinyanga (1984) Limited kilisambaza tani 1,000 za
mbegu za pamba zenye thamani ya shilingi 45 milioni wakati wakijua kuwa
ni uongo.
Matondo alikana shitaka hilo na upande wa
mashitaka ulidai kuwa upelelezi wake bado haujakamilika na Hakimu Simba
alihairisha kesi hiyo hadi Julai 28, 2015 .
Mshitakiwa huyo alishidwa kukamilisha
mashariti ya dhamana na kutakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika
na kutoa Shilingi 20 milioni.
Post a Comment Blogger Facebook