0
Habari za masiku ndugu msomaji, pole kwa pilika pilika za maisha na kazi za hapa na pale. Leo hii nimewaletea uchambuzi mdogo wa video mpya ya wimbo ‘Kuliko Jana’ ya wasanii wanaofanya vizuri kutoka nchini Kenya, Sauti Sol.
sauti-sol-kuliko-jana-featuring-redfourth-chorus-upper-hill-school
Kama bado haujaingialia video hii hebu itafute mara moja, kwaani huwenda ikawa ni video yako bora ya muziki ndani ya mwaka 2016 kutokana na uburibu mkubwa uliotumika katika kuandaa kazi hiyo.
Video ya ‘Kuliko Jana’ imeandaliwa na madirector wawili wa nchini Kenya, Joash Omondi pamoja Mwaura Timothy ambao wamefanya kazi kubwa katika kuonganisha wazo la kufikirika na kuliweka katika video.
Wimbo ‘Kuliko Jana’
Naamini kama hauna wimbo mzuri basi hata video itakuwa yamashaka mashaka, lakini wimbo ‘Kuliko Jana’ ni wimbo ambao unazungumzia maisha ya watu pamoja na kumwamini Mungu katika maisha. Watu wamechoshwa na hali ya maisha, magonjwa, dhiki na mambo mengine, wanataka nyimbo ambazo zinazungumzia maisha yao pamoja na kuwatia moyo, ndio maana mashabiki wengi kupitia mitandao ya kijamii wameonyesha kuukubali wimbo ‘Kuliko Jana’.

Video ‘Kuliko Jana’

Tumeona video za wasanii wengi wa Afrika Mashariki toka mwaka uanze lakini video ya ‘Kuliko Jana’ ni kiboko. Ladha ni kutokana na ushirikiano wa madirector wawili ambao wameonyesha ubora wa picha. Pia light, jinsi short moja na nyingine zinavyopishana, location pamoja na wingi wa watu walioshiriki kwenye video ni moja ya vitu ambavyo vinavutia sana kwenye video.
Video hiyo ambayo ina siku 5 toka itoke tayari kupitia YouTube ina views zaidi ya laki 233,000 kuhu ikiwa na komenti zaidi ya 1500. Hii ni hatua nzuri ambayo imetokana ubunifu mkubwa ambao umefanyika katika kuandaa video hiyo.
Komenti nyingi za YouTube zionyesha ni jinsi gani mashabiki wameikubali kazi hiyo, huku mashakibi wengine wa mashariki ya mbali wakiomba kutafsiriwa kutoka na lugha ya Kiswahili iliyotumika kushindwa kuitambua.
Kuna msemo usemao muziki ni lugha ya dunia, na ubunifu ni kitu kipekee ambacho kinaweza kuufikisha muziki hata sehemu usiyoipanga, PSY kutoka South Korea aliweza kufanya mambo makubwa na wimbo ‘Gangnam Style’ na kuvunja rekodi mbalimbali za dunia kutokana na kufanya kitu tofauti katika macho ya watu. Hata wewe unaweza kufanya maajabu, amka sasa.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top