Mvutano umeibuka kati ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson na wasemaji wa kambi ya upinzani walipokuwa wakisoma maoni yao kuhusu miswada iliyowasilishwa bungeni baada ya kusoma utangulizi uliokuwa nje ya hoja.
Katika
Bunge la Bajeti lililoisha Juni mwaka huu, upande wa Kambi ya Upinzani
Bungeni uliingia kwenye mgogoro na Dk Tulia, hali iliyosababisha wabunge
kutoka vyama vinavyounda Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi) kutoka
bungeni kila Naibu Spika alipokuwa akiendesha vikao.
Jana,
ilikuwa mara ya kwanza tangu wabunge wasusie vikao vinavyoendeshwa na
Dk Tulia kukubali kuwapo ndani ya Bunge, hatua iliyotokana na viongozi
wa dini kuingilia kati sakata hilo.
Tangu
kuanza kwa Mkutano wa Nne wa Bunge la 11, imepitishwa miswada miwili
huku wapinzani wakisoma utangulizi wa maoni kueleza jinsi wanavyobanwa
kufanya shughuli za siasa.
Hata
hivyo, jana ilikuwa ni tofauti baada ya Dk Tulia kuwabana wawasilishaji
wa miswada ya Sheria ya Uanzishaji wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu
wa Serikali, ambao ulisomwa na Dk Godwin Mollel na aliyesoma Muswada wa
Uanzishaji Baraza la Watalaaluma wa Kemia ni Ester Matiko.
Katika
maoni yao, Matiko na Dk Mollel walieleza jinsi Polisi na Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanavyowapiga na kuwakamata wananchi
wanaojadili masuala ya siasa. Dk Mollel alipinga watu kunyimwa haki ya
kutoa maoni, kufanya mikutano ya hadhara na maandamano. “Tupinge unyama
unaondelea dhidi ya Watanzania wenzetu,” alisema Dk Mollel.
Hata
hivyo, kabla ya kumaliza kile alichokuwa akitaka kusema Naibu Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu), Dk
Abdallah Posi aliomba mwongozo kwa kutumia kifungu namba 68 (1) akitaka
msemaji kujielekeza katika hoja kama kinavyotaka kifungu 86.
Baada
ya Dk Tulia kutoa mwongozo wa kutaka kuacha kusoma maneno ya utangulizi
huo, Dk Mollel alitii na kuendelea na hoja iliyokuwa mezani.
Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya Matiko kuingia kusoma maoni ya kambi hiyo kuhusu Muswada wa Sheria ya Uanzishwaji wa Baraza la Wanataaluma wa Kemia.
Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya Matiko kuingia kusoma maoni ya kambi hiyo kuhusu Muswada wa Sheria ya Uanzishwaji wa Baraza la Wanataaluma wa Kemia.
“Watanzania wote wenye mapenzi mema tupinge vyombo vya dola vinavyotumika kufanya shughuli za siasa,” alisema Matiko.
Licha ya Dk Possi kuomba mwongozo wa Spika, Matiko aliendelea kusoma maneno ya utangulizi ambayo aliambiwa asiyasome.
Wakati
mvutano huo ukiendelea, baadhi ya wabunge wa upinzani walisimama
kupinga uamuzi wa Dk Tulia wakitaka wasemaji hao kuendelea kusoma
utangulizi.
Hata
hivyo, Dk Tulia aliwataka kukaa chini huku akimtaja Mbunge wa Kawe
(Chadema), Halima Mdee kwa zaidi ya mara mbili akimsihi kukaa hali
aliyokubaliana nayo.
Post a Comment Blogger Facebook