Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
ameiagiza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nchi kuchunguza na
kuwachukulia hatua kisheria na za kinidhamu viongozi na watumishi wa
umma ambao wanakiuka taratibu za kazi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 8-Sep-2016 mjini Mtwara
wakati anafungua jengo la sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma
Kanda ya Kusini ambalo ujenzi wake umegharimu takribani shilingi bilioni
MBILI.
Makamu
wa Rais amesema iwapo kama hatua hizo zitachukuliwa haraka zitakomesha
na kupunguza kasi ya mmomonyoko wa maadili kwa viongozi na watumishi wa
umma hali ambayo itaongeza uwajibikaji katika utendaji wa kazi miongoni
watendaji hao.
Amesisitiza
kuwa serikali itaendelea kuiimarisha sekretarieti ya maadili ya
viongozi wa umma nchini kwa kuijengea uwezo wa rasilimali watu na fedha
kwa kadri hali ya uchumi itakavyo ruhusu ili waweze kutekeleza majukumu
yao kwa ufanisi.
Makamu
wa Rais amewahimiza viongozi na watumishi wa umma kuthamini na
wahakikishe walinda maslahi ya umma wakati wote wa utendaji wao wa kazi
ili kuondoa malalamiko kwa wananchi.
Makamu
wa Rais amesema ni jambo la muhimu kwa sekretarieti hiyo kufutilia
mienendo ya viongozi wa umma na kuwabaini wale wanaokwenda kinyume na
misingi ya uadilifu na wachukuliwe hatua ipasavyo kabla hawaleta madhara
kwa serikali na jamii kwa ujumla.
Makamu
wa Rais pia ametoa rai maalum kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara kuitumia
ofisi hiyo mpya ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya
Kusini kwa kutoa taarifa kuhusu mienendo ya viongozi wanaokiuka maadili
ya umma katika utendaji wao wa kazi ili waweze kuchukuliwa hatua.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala bora Angela Kairuki amesisitiza kuwa kazi ya kuhakiki
mali na madeni ya viongozi wa umma itaendelea kwa kasi nchini na mwaka
huu sekretarieti hiyo itahakiki mali za viongozi wapatao 500 kote
nchini.
Naye
Jaji Mstaafu na Kamishna wa Maadili Nchini Salome Kaganda akitoa
taarifa kuhusu ujenzi wa jengo hilo ameiomba serikali itenge fedha za
kutosha kwa ajili ya kufanikisha zoezi la uhakiki wa mali na madeni ya
viongozi kwa nchi nzima.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Mtwara.
8-Sep-2016.
Post a Comment Blogger Facebook