Na Sheila Simba- MAELEZO
Waziri
wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa
Serikali imeanza kazi ya kupima ardhi nchi nzima kuanzia mkoani
Morogoro.
Akizungumza
katika kipindi kipya cha "TUNATEKELEZA" kinachoandaliwa na Idara ya
Habari-MAELEZO na TBC1 ,alisema utekelezaji wa zoezi hilo umeanzia
mkoani humo ili kupima maeneo ya wakulima na wafugaji na kutatua
migogoro ya ardhi Mkoani humo.
“Serikali
tumedhamiria kumaliza migogoro ya ardhi, kutimiza ndoto ya Rais
Magufuli ya kuondokana na migogoro ya ardhi isiyo na tija inayosababisha
watu kupoteza maisha’’Alisema Lukuvi
Ameongeza
kuwa katika upimaji huo wa ardhi serikali inashirikiana na kampuni
binafsi zilizosajiliwa ili kumuwezesha mwananchi anayemiliki
shamba,kiwanda ,mkulima na mfugaji mwenye eneo kupimiwa na kuongezewa
thamani.
“Nakuhakikishia
katika kipindi cha miaka 10 kila kipande cha ardhi Tanzania kitakuwa
kimepangwa na kupimwa utaratibu mzuri utakao mwezesha kila mtumiaji wa
ardhi kutumia eneo lake”alifafanua Lukuvi.
Pia
ameeleza suala la kuthibiti bei ya kupima ardhi kwa kushirikiana na
wapimaji binafsi katika kumfanya kila mtanzania alipe bei halali ya
kupima ardhi.
Aidha
amesme kuwa Serikali itaweka ukomo wa kumiliki ardhi ili kuondoa tabia
za watu kumiliki eneo kubwa la ardhi bila ya kuliemdeleza kwa muda
mrefu.
“serikali itaweka muda wa mtu kumiliki ardhi, haiwezekani mtu mmoja amiliki eneo hata bila kulitumia, tabia hii itafika mwisho.”
Akizungumzia
suala la wageni kumiliki ardhi alisema kuwa ni marufuku kwa wageni na
wawekezaji kununua ardhi vijijini bila kupitia wizara inayohusika.
“Ni
marufuku kwa mgeni au mwekezaji kwenda kijijini kununua ardhi bila kuja
kwangu au Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),wakifanya hivyo tutawapa
ardhi wawekeze, Pia mtu yeyote anayetaka kujenga kiwanda popote afike
ofisini kwangu nitampatia ardhi ndani ya siku saba.”alisema Lukuvi
Ameongeza
kuwa Wizara imetenga viwanja 240 kwa ajili ya Viwanda enoa la
Kigamboni ili kutimiz lengo la Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.
Mbali
na hayo Waziri Lukuvi alisema wananchi wote waliodhulumiwa viwanja
Jijini Dar es Salaam kwa makosa ya watendaji wa Serikali wameanza
kupewa viwanja vingine mbadala.
“Naagiza Halmashauri zote ziwapatie viwanja mbadala wananchi ambao walidhulimiwa viwanja vyao kwa makosa ya watendaji.”
MWISHO
Post a Comment Blogger Facebook