chibwa |
Amesema hiyo ndiyo sababu kwa sasa atakuwa akifanya nyimbo zake kwa Kiingereza zaidi ili kuwafikia watu wengi.
?Nia yangu ni kubadilisha muziki wa kitanzania nisiimbe lugha ya Kiswahili kabisa,? Chibwa alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM Alhamisi hii.
?Nimeshaanza kufanya track za namna hiyo, nimefanya track na Chris Martin ambayo ni track yangu ya kwanza ambayo nimetumia lugha ya Kiingereza. Mimi na maproducer pamoja na timu yangu kwa sasa hawatamani tena niimbe nyimbo kwa Kiswahili, nipo naendelea kufikiria nyumbani ni nyumbani na worldwide ni worldwide tu, kwa sababu nataka hela yenye sura ya mtu mwingine sio yule ambaye nimemzoea kumuona, kwahiyo nitaishika vipi? Inabidi niisogelee kwa jinsi wao wanavyotaka, niisogelee ili iwe karibu nami,? alisisitiza.
Aliongeza, ?Kwahiyo nipo na timu yangu tunajadili zaidi tuendelee kuziokotaokota pesa za Magufuli au tumkimbie tukatafute mbele.?
Post a Comment Blogger Facebook