0
CHOMBEZO: KITANDA CHA MAMA MWENYE NYUMBA....SEHEMU YA.... 01
Mtunzi_Na: IRENE MWAMFUPE NDAUKA

“Mke wangu, kilasiku namwona huyu kijana mchafuchafu anakuja kuokotachupa tupu hapa, ina maanatuna chupa tupu kila siku?”“Siyo hivyo mumewangu, we hujamfuatilia tu, anakuja kila baada ya siku tano. Tumsaidie mume wangu,si unamwona kijana mwenyewe masikini huyu,” alisema mama Joy huku macho yakeyote yakimwangalia yule kijana mwokota makopo…“Awe anakujamchana basi, usiku kama huu hapa nje, mimi naweza kumchapa risasi nikidhanimwizi. Si unaona hata mavazi yake? Kwanza haogi huyu, hata harufu anatoa…”“Mume wanguusimkufuru Mungu, sisi kupewa uwezo ni matakwa yake, hakuna binadamu ambayeakipewa nafasi ya kuchagua maisha bora na duni, atasema anataka duni.”“Mimi sijafikahuko, ila nasema awe anakuja mchana tu si usiku kama huu.”“Sawa mume wangu,”alisema mama. Hayo yalitendeka wakatibaba Joy akiegesha gari mahali pake kisha akashuka na kuanza kutembea mkononiameshika brifkesi yake. Siku hiyo, baba Junior alikuwa kama amevaa Kinaijeriaf’lani.Mama Joy alimpokesamumewe brifkesi kisha akamwacha apite ili yeye amfuatekwa nyuma. Wakati mumeweanaingia, mama Joy aligeuka kumwangalia mwokota chupa tupu ambaye kwa muda huoalikuwa amebeba fukp la ‘salfeti’ begani.Mama Joyalimwonesgha ishara kwamba aondoke haraka sana kwa vile mumewe amerudi. Kijanawa watu, alitoka getini kwa kuruhusiwa na mlinzi.“Unasikia mamaJoy,” baba Joy alianza kusema tena akiwa amekaa kwenyesofa kubwa…“Abee…”“Mimi sipendi watuwawe wanaingiaingia humu ndani hovyo. Tena nadhani iko haja ya sehemu yakutupia taka niijenge nje ili watu wasipate sababu ya kuingia ndani…“Wewe kijanamchafuchafu vile, si lazima pia atakuwa mwizi..?”“Nimekuelewa babaJoy, hataingia tena usiku ikitokea itakuwa mchana.”“Iwe hivyo, sitakikumwona tena usiku. Kwanza wewe ni mke wa mtu, mnachekeanachekea kwa sababugani?”“Basi mume wangujamani, nimekuelewa.”Mzee huyo aliondoka kwenda kazini, mkewemama Joy alisiama nje kwa muda mrefu, alipotaka kugeuka kurudi ndani, kwa mbalialimwona mwanaume akitokea. Mgongoni alibeba furushi…“Au yule?” alisema moyoni. Alisubiri kwamuda ili amwone kwa karibu, lakini hakuwa yeye.Nusu saa baada ya kuingia ndani, kengele yageti kubwa ililia…“Mh! Si yeye huyo?” alijihoji mama Joyakiamini aliyebonyeza kengele ni mzoa taka. Japokuwa alijua mlinziatashughulikia, lakini aliamua kutoka mwenyewe kuelekea getini ambapo alimkutamlinzi anasukuma geti kubwa.“Naniamepiga kengele?” mama Joy aliuliza…“Sijamjua ni nani?” mlinzi alijibu hukuakiendelea kusukuma geti, likawa wazi…“Shikamoo mama,” mzoa taka alisalimia akiwaanatabasamu...“Hujambo wewe?”badala ya kusema marhaba. Na tangu mzoa taka huyo ameanza kuingia ndani yanyumba hiyo kuchukua taka, kila akimsalimia shikamoo mama Joy anajibiwa hujambowewe au asante kijana…“Sijamboo, shikamoo…”“Asante…askari, funga geti…”“Sawa. Huyu mzoa taka aingie..?”“Aingie ndiyo. Akishaingia funga geti.”Mzoa taka aliingia hadi ndani, akamkaribiamama Joy ambaye naye alimkaribisha hadi kwenye sehemu yenye taka.Mlinzi aliwakodolea macho. Kilichomshangazazaidi ni kauli ya baba Joy kwamba hataki kumwona mlinzi huyo nyumbani kwake…“Sasa mbona amemuingiza tena leo? Halafukuna siri nzito mimi naiona kati ya mama na huyu mzoa taka, maana mamaakiamkiwa shikamoo hatakagi kuitika marhaba,” mlinzi aliwaza.Mama Joy alimfikisha mzoa taka kwenye pipala taka ambalo lilijengwa vizuri ndani ya nyumba hiyo…“Jana mwenzangu mzee alikasirika sana,”alianza kusema mama Joy…“Hata mimi kama nilimwona. Niliogopa sana…”“Yeye anasema hataki kuona unaingia humundani usiku.Akasema atalitoa hili pipa na kulijengea nje huko.”“Kwa hiyo akinikuta saa hizi humu ndanikwake si ataniua?”“Hawezi, ingawa ana bastola…”“Mama mimi nakwenda, kumbe mumeo anabastola..!”“Hawezi kukuua, alisema hataki uingie usiku,‘asa kwani saa hizi ni usiku?”JE NINI KITAENDELEA...USIKOSE...SEHEMU YA ....02.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top