Mamlaka
ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetoa adhabu ya onyo kali na
kukitaka kituo cha ITV kuomba radhi mara mbili mfululizo kwenye
taariifa zake za habari baada ya kukiuka sheria ya utangazaji nchini ya
Mwaka 2005.
Hukumu
hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya
utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Margaret Munyagi (pichani) wakati wa Mkutano na Waandishi
wa Habari ambapo Muyangi alisema kamati hiyo imebaini kituo cha ITV
kulikiuka sheria hiyo ya utangazaji nchini kwa kurusha taarifa ambayo
ingeweza kuleta machafuko nchini.
Alidai
katika kipindi cha Habari zilizotufikia muda huu kilichorushwa siku ya
Jumatatu ya tarehe 10 mwezi huu majira ya saa 2.22 asubuhi , ITV
Walitangaza “Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga
marufuku maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakati
wa kumsindikiza Lowassa kwenda kuchukua fomu ya Urais."
Alisema
katika kipindi hicho Mtangazaji wake alisikika akisema Jeshi hilo
limezuia maandamano hayo baada ya kubaini yanauvunjifu wa amani huku
Mtangazaji huyo akimnukuu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam Suleiman Kova akidai ndo amesema hivyo,Wakati taarifa hiyo
ilikuwa ya upotoshaji kwani jeshi hilo halikuwa limetoa taarifa hizo..
Bi
Muyangi alisema baada ya ITV kurusha taarifa hiyo ya kwanza juu
kuzuiliwa huko kwa maandamano, ndipo siku hiyo hiyo tena katika
kipindi hicho cha Habari zilizotufikia mda huu majira ya saa tatu
asubuhi kilirushwa taarifa inayosema Jeshi la Polisi limeruhushu
maandamo ya Chadema kutoka Makao makuu wa Chama cha Wananchi CUF
Buguruni Jijini Dar es Salaam kwenda Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
NEC.
Muyangi
alidai katika taarifa hiyo ilisikika sauti ya Kamanda Kova juu ya
kuruhusu maandamono hayo,tofauti na taarifa ya kwanza ambayo haikuweka
uthibitisho wa Kamanda Kova.
Alisema
baada ya Mamlaka hiyo kubaini makosa hayo,Kamati hiyo iliwasiliana na
Mkurugenzi wa ITV Bi Mhavile na mkurugenzi wa Redio one Deogratus
Rweyunga pamoja na Mhariri wa ITV Steven Chuwa ili kutaka ufafanuzi
ambapo wote kwa pamoja walikiri kosa hilo huku wakisema Mtangazaji huyu
alitoa taarifa kwenye Mitandao ya Kijamii ambayo ilikuwa inakataza
maandamano hayo ambapo alishindwa kuithibitisha kama taarifa hiyo ni
ya kweli au la.
Aidha,
Bi Muyangi alisema baada ya Kamati hiyo kusikiliza pande zote,ndipo
wakatoa hukumu kwa kupitia sheria ya Utangazaji ya mwaka 2005 ambayo
inakataza kituo chohote cha Utangazaji kurusha taarifa zinazoleta
mchanganyiko katika jamii,
Post a Comment Blogger Facebook