Jeshi
la Polisi nchini limesitisha maandamano ya aina yoyote wakati wote wa
zoezi la kuchukuwa fomu, kutafuta wadhamini mikoani na hata wakati wa
kurejesha fomu ili kuweka hali ambayo haitaleta usumbufu au kuhatarisha
usalama wa raia na mali zao.
Akitoa
taarifa hiyo jana mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
naibu inspekta jenerali wa polisi Abdulrahman Kaniki alisema uamuzi huo
umefikiwa baada ya jeshi hilo kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi
juu ya usumbufu uliojitokeza wa watu kushindwa kuingia maofisini na
wengine kushindwa kufika kwa wakati katika shughuli za kiuchumi na
kijamii kutokana na misafara mirefu iliyosababishwa na vyama vya Chadema
na CCM wakati wagombea wao walipokwenda kuchukuwa fomu.
Aidha
amesema jeshi hilo halina ugomvi na chama chochote cha siasa wala
mchakato wa uchaguzi unaoendelea isipokuwa lengo lao ni kutengeneza
mazingira mazuri ili vyama vyote viweze kutekeleza majukumu yao vizuri
na kwa kufuata sheria za nchi.
Akijibu
maswali mbalimbali ya waandishi wa habari likiwemo la tuhuma
zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na ambazo baadhi ya wanasiasa
wanazizungumzia juu ya askari polisi kutakiwa kupeleka shahada zao za
kupigia kura ili namba zao za uandikishwaji zichukuliwe naibu inspekta
kaniki alisema swala hilo halina ukweli wowote.
Post a Comment Blogger Facebook