TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI
Leo
tarehe 6 Agosti, 2015 Profesa Ibrahim Lipumba aliitisha mkutano na
waandishi wa habari katika Hoteli ya Peacock, mjini Dar es Salaam na
kutangaza kwamba amejizulu nafasi yake kama Mwenyekiti wa Taifa wa Chama
Cha Wananchi (CUF).
Sisi
kama Chama tumezipokea taarifa hizo na tunayaheshimu maamuzi yake. Ni
haki yake ya kikatiba na haki ya kidemokrasia kufanya maamuzi anayoyaona
yana maslahi kwake.
Bila
shaka, Profesa Ibrahim Lipumba amekifanyia kazi kubwa Chama chetu
katika miaka 16 ambayo alikuwa Mwenyekiti wetu, nafasi iliyomfanya awe
kiongozi wetu mkuu. Kwa nafasi yake hiyo, pia ametoa mchango mkubwa
katika ujenzi wa demokrasia katika nchi yetu. Tunaithamini kazi hiyo na
tutaendelea kumheshimu kwa utumishi wake mkubwa kwa Chama chetu na nchi
yetu. Tunamtakia kila la kheri katika mipango yake ya baadaye.
Chama
Cha Wananchi (CUF) ni taasisi na kinaendeshwa kitaasisi. Ndiyo maana
maamuzi yake yote yamekuwa yakifanywa kitaasisi kwa mujibu wa Katiba na
Kanuni za Chama. Kwa msingi huo, pamoja na ukweli kwamba kuondoka kwa
Profesa Lipumba katika safu ya uongozi kutaacha pengo hasa katika
kipindi hichi ambacho tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, tunawahakikishia
wanachama na wapenzi wa CUF na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwamba
Chama hichi hakitayumba.
Katika
historia yake, CUF imepita katika dhoruba na misukosuko mingi lakini
mara zote kimeonesha uwezo mkubwa wa kuhimili dhoruba na misukosuko hiyo
na kukabiliana na athari zake. Hatuna chembe ya wasiwasi kwamba hata
mtihani huu tutauvuka na tunaamini tutaibuka tukiwa Chama imara zaidi.
Katibu
Mkuu ameagiza kuitishwa kwa vikao vya dharura vya Kamati ya Utendaji ya
Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa siku ya Jumapili, tarehe 9
Agosti, 2015 ili kujadili hatua hiyo na kufanya maamuzi juu ya hatua
muafaka zinazopaswa kuchukuliwa katika kipindi hiki hadi hapo Chama
kitakapomchagua mwanachama mwengine kujaza nafasi hiyo ya Mwenyekiti.
Katika
kipindi hiki, Chama kinawataka wanachama na wapenzi wake wote kuwa
watulivu na wavumilivu na kusubiri maelekezo ya vikao vya juu vya
kitaifa vya Chama.
Mwisho
kabisa, tunawahakikishia wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla
kwamba CUF itaendelea na shughuli zake kama Chama na pia kama mshirika
katika UKAWA ambayo CUF ilikuwa ni katika waasisi wake.
Tunawahakikishia wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla kwamba CUF itatumia nguvu, uwezo, juhudi na maarifa yake yote kuhakikisha kwamba inaulinda UKAWA ambao unaonekana kuwa mwiba kwa CCM.
Tunatambua kwamba kuna njama na mbinu kubwa na nyingi zinazofanywa na watawala kutaka kuuvuruga na kuuhujumu UKAWA wakidhani kwamba watapata manusura.
Tumesema na tunaendelea kusema CCM mwaka huu hawana manusura.
Watanzania wameamua kuwan’goa, na watan’goka Tanzania Bara na Zanzibar kupitia sanduku la kura tarehe 25 Oktoba, 2015. Wimbi hili kubwa la mabadiliko halizuiliki tena.

HAKI SAWA KWA WOTE
ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO NA UMMA
06 AGOSTI, 2015
Post a Comment Blogger Facebook