Ukumbi mpya wa CCM mkoani Dodoma.
Baadhi ya wanachama wa CCM walijitokeza kuhudhruria uzinduzi huo.
Maandalizi ya uzinduzi wa ukumbi wa CCM.
Wanachama CCM wakati wa maandalizi ya uzinduzi wa ukumbi mpya.
Kinachoendela Mkoani Dodoma hivisasa ni maandalizi ya uzinduzi ukumbi mpya wa CCM uliopo njia ya kwenda chuo kikuu cha Dodoma.
Wageni mbalimbali wamehudhuria uzinduzi huu ambapo Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ndiye atakayezindua ukumbi huo lakini hadi sasa bado hajawasili katika ukumbi huu mpya na wa kisasa.
|
Rais Kikwete akikagua moja ya ukumbi wa kisasa uliopo katika majengo ya ukumbi mpya wa CCM mkoani Dodoma.Add caption |
Kwa upande mwingine, leo mchana kutakuwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi ambayo nayo ni muendelezo wa vikao vya awali kuelekea mkutano mkuu.
|
Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amesema kwamba maarifa mafupi ya viongozi CCM ndio kikwazo kikubwa cha chama kushindwa kujipatia kipato kutokana na kuwa rasilimali nyingi mfu kuliko chama chochote cha siasa nchini Tanzania ambazo hazijaweza kukizalishia chama kipato.
Kikwete amesema hayo leo wakati akizindua jengo jipya la CCM lilipo barabara ya kwenda chuo kikuu cha Dodoma ambalo limejengwa mahusisi kwa ajili vikao vya chama pamoja na chama kujiongezea kipato kutokana na kulikodisha jengo hilo kwa matumizi mengine.
“Ukumbi huu utatumika mara mbili tu kwa mwaka hivyo hautakaa tu usubiri vikao hivyo, utakodishwa kwa watu wengine ambao watailipa CCM”.Amesema Rais Kikwete.
Ameongeza kuwa CCM ina rasilimali nyingi ikiwemo viwanja katika maeneo mbalimbali nchini, rasilimali hizo zimekuwa zikigawanywa kwa viongozi wa mikoa pamoja na mapato yake kutia mfukoni.
Ametolea mfano jijini la Dar es salaam CCM ina viwanja taribani 420 ambavyo havija endelezwa na matokeo yake kutumika kulazia magari na walinzi kujichukulia mapato yanayopatikana.
Amewataka viongozi wa chama hicho kuingia ubia na makampuni ya ujenzi ili kuendeleza maeneo hayo kwa mkataba utakao zinufaisha pande zote mbili.
Amesisitiza kuwa viwanja vya CCM sasa vibadilike kutoka rasilimali mfu hadi kuwa rasilimali zinazotoa na kukuza mtaji.
Ukumbi huo una uwezo wa kuchukua wajumbe takribani 3000 ukiwa na ukumbi mkubwa pamoja na kumbi nyingine ndogo ndogo huku ukiwa na sehemu pana ya maegesho ya magari.
|
Post a Comment Blogger Facebook