0
Mchazaji Jerome Nturukindo Baraka (Kulia)akiwa na wakala wake Othman Noor
Watanzania wameonekana kushika kasi katika soka la kimatiafa baada ya kijana  Jerome Nturukundo Baraka kufuzu majaribio yake katika timu ya Partizan Belgrade inayoshiriki ligi kuu nchini Serbia.

KInda huyo ambaye alishawa kushiriki mashindano ya  Copa Coca Cola kwa mkoa wa Temeke mwaka 2011 ameonekana kuwavutia zaidi timu hiyo ya Partzan Belgrade.

Wakala wa mchezaji huyo Othman Noor ambaye ni raia wa Kenya almesema Jerome ameweza kuwavutia timu hiyo na wako tayari kumsajili mwezi Januari 2016.

Amesema watamuangalia kwa muda huu uliobaki na watatuma mtu maalumu kuja kuangalia maendeleo yake ya kimpira kabla ya kuja kucheza soka la ushindani katika nchi yao.

Mchezaji huyo ambaye aliwahi kuichezea timu ya U20 ya African Lyon kwa mwaka 2012/13 anatarajia kurudi nchini kuja kufanya mazungumzo na timu mojawapo inayocheza ligi kuu Tanzania Bara.

Noor ameongeza mpaka sasa ameshafanya mawasiliano na timu ya Simba kwa ajili ya kumpa nafasi kijana huyo mpaka hapo timu ya Partzan Belgrade kumsajili mwanzoni mwa mwaka 2016.

Hivisasa

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top