Azam FC inatarajia kumpokea mlinda lango Mkameruni anayekipiga nchini DRC Nelson LUKONG – leo saa nne usiku na Kenya Airways
Mbali na Nelson LUKONG, kesho saa mbili asubuhi kiungo toka nchini England Ryan Burge atawasili na Qatar Air.
Kesho hiyohiyo majira ya saa kumi nyakati za jioni Jean Mugiraneze Babtiste toka nchini Rwanda anayekipiga na APR atawasili na Rwanda Air
Baada ya mazoezi ya wiki tatu Azam FC inasafiri kesho asubuhi kuelekea mjini Tanga kucheza mechi mbili za kirafiki. Itacheza na African sports wana kimanumanu siku ya Jumamosi na Jumapili itakwaana na Coastal Union Mechi zote mbili zitachezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani majira ya jioni.
Timu itarejea Dar es Salaam siku ya Jumatatu.
Post a Comment Blogger Facebook