MAHABUSU Watatu waliokuwa wanapelekwa katika Gereza la
Butimba, jijini Mwanza, wakitokea kijiji cha Nyang`amango wilayani
Misungwi, wamefariki dunia wakati wakijaribu kuwanyang`anya Polisi
silaha. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Japhet Lusingu, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema, Ebina Muhono, Mkazi wa Mkuyuni jijini hapa, alikufa papo hapo baada ya kuruka kutoka kwenye gari la Polisi namba PT. 1680 Land Cruiser.
Amesema wengine wawili, Daniel Elias na Maramba Range, wao
walipata majeruha baada ya kuanguka wakati wakijaribu kuruka na
kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi na walifariki dunia
jana asubuhi.
Lusingu amesema katika tukio hilo ambalo lilitokea Julai 23
Mwaka huu saa 10:30 jioni, mahabusu mmoja, Denis Mahuti, Mkazi wa
Tarime alifanikiwa kutoroka akiwa chini ya ulinzi wa sajenti, Mahamoud.
“Mahabusu hao ghafla walijaribu kuwapora askari silaha
waliokuwa wakiwasindikiza katika gereza la Butimba lakini Polisi
walipambana na watuhumiwa na kushindwa kuwapora silaha,” amesema
Lusingu.
Hata hivyo amesema watuhumiwa wote wanne wanatuhumiwa kwa
kesi za unyang`anyi wa kutumia silaha ambazo ni CC. 27 na 30 za Mwaka
2015 katika Mahakama ya Wilaya ya Misungwi.
Wakati huo huo, watu wanne wanaodaiwa kuwa majambazi
waliokuwa na silaha idhaniwayo ni SMG/ SAR wamevamia boti ya Mv.
Zenegathe na kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja
la Charles.
Kamanda Lusingu amesema tukio hilo lilitokea Julai 23 Mwaka
huu, saa 9:00 katika kisiwa cha Goziba kilichopo Mkoa wa Kagera na
kisiwa cha Ghana
Post a Comment Blogger Facebook