0

Shambulizi la awali la Boko Haram mjini Maiduguri

Wakati huo huo,miili zaidi inaendelea kufukuliwa kwenye vifusi vya nyumba zilizoharibiwa  na shambulizi linaloshukiwa kutekelezwa na Boko Haram wiki iliyopita kaskazini mashariki mwa Nigeria.  
Mlipuaji bomu wa  kujitoa mhanga ameua takriban watu watano kwenye kanisa lililoko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Shambulizi hilo ndilo la karibuni zaidi kwenye mashambilizi ambayo yanashukiwa kufanywa na kundi la Boko Haram na ambayo yamewaacha watu 200 wakiwa wamepoteza maisha katika kipindi cha wiki moja iliyopita.
Mlipuko huo umetokea jumapili asubuhi kwenye kanisa lililoko Potiskum mji mkubwa ulioko katika jimbo la Yobe. Walioshuhudia wanasema mlipuaji bomu alijidai kuwa muumini wa kanisa hilo na kisha kutegua kilipuzi muda mfupi baada ya kuingia kanisani.
Shambulizi hilo linafuatia jingine lililotokea ijumaa karibu mji mkuu wa jimbo la Borno,Maiduguri. Maafisa wa kijeshi wanasema kuwa wanawake sita walipuaji mabomu wa kujitoa mhanga walisababisha milipuko na kuua darzeni ya watu akiwemo mwanajeshi mmoja.
Wakati huo huo,miili zaidi inaendelea kufukuliwa kwenye vifusi vya nyumba zilizoharibiwa  na shambulizi linaloshukiwa kutekelezwa na Boko Haram wiki iliyopita kaskazini mashariki mwa Nigeria.  

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top