
Polisi mjini Mwanga, mkoani Kilimanjaro umezuia msafara wa mgombea urais
kupitia Chadema, Edward Lowassa uliokuwa unaelekea Usangi kuhudhuria
mazishi ya kada wa CCM, Peter Kisumo.
Vyanzo vya kuaminika toka mjini Mwanga vinasema, polisi walizuia msafara
huo kutokana na kujumuisha idadi kubwa ya magari ya viongozi waandamizi
wa Ukawa na wabunge wanaounda umoja huo jambo ambalo polisi
hawakuafiki.

Taarifa zinasema, tukio hilo lililotokea katikati ya Mwanga na Usangi
lilizusha mjadala wa zaidi ya dakika 30, polisi wakitaka Lowassa aende
mazishini peke yake huku magari mengine yaliyoambatana naye yarejee
yalikotoka jambo ambalo halikuafikiwa na mwanasiasa huyo.

Baada ya polisi kusisitiza kutoruhusu msafara mzima uende mazishini
mgombea huyo aliamua yeye na maofisa wengine alioambatana nao kurudi
Mwanga akisisitiza asingeweza kwenda peke yake akiwaacha watu
aliambatana nao.
Post a Comment Blogger Facebook
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.