Muimbaji wa RnB kutoka Marekani, Trey Songz anatarajiwa kuungana na wasanii wengine wa Afrika ambao watashiriki kwenye msimu wa nne wa kipindi cha Coke Studio Africa.
Uongozi wa kipindi hicho umeandika ujumbe kwenye mtandao wao wa Instagram unaosomeka, “BREAKING NEWS: Joining Coke Studio Africa Season 4 is singer, songwriter, record producer and actor… @treysongz! Follow the conversation on #CokeStudioAfrica.”
Hii ni mara ya tatu kwa msanii kutoka Marekani kushiriki kwenye kipindi hicho. Wyclef Jean na Ne-Yo nao wamewahi kushiriki.
Kwa upande wa wasanii wa Tanzania waliochaguliwa kushiriki kwenye kipindi hicho kwa msimu huu ni pamoja na Vanessa Mdee, Joh Makini, na Yamoto Band huku Diamond akishiriki ile ya Afrika Kusini (Coke Studio ZA).

Post a Comment Blogger Facebook