0
Mtunzi : EDDAZARIA G.MSULWA
 Mioyo ya watu wengi wanao jishuhulisha nje ya eneo hili la Benki hii ya kijamii baada ya kundi la wasichana wapatao watano wakiwa na  bunduki zenye uwezo mkubwa wakiwa na kazi moja iliyo wapeleka katika eneo hili ambayo si nyingine zaidi ya kushambulia askari yoyote atakaye jipendekeza katika shuhuli ya uibaji wao wa fedha ambao wameidhamiria kwa siku nyingi na leo ndio hitimisho la mipango yao.Wamejitolea kufa na kupona huku kila mmoja akiwa makini sana na upigaji wake wa risasi zinazo toka kweye unduki zao za kila aina.
Wasichana wawili wakaingia ndani na mkuwalaza chini wahudumu wote wa benki pamoja na wateja ambao wapo ndani ya benk hii na hawakuwa na huruma kwa yoyote aliye inyanyua shingo yake kwa madai ya kuwatazama ni kina nani ambao wanafanya kazi hiyo na ambaye alijaribu kufanya hiyo basi risasi kadhaa kama si mbili basi ni zaidi ya mbili zinatua kwenye mwili wake
Wakamkamata meneja wa benki na kumuamrisha awapekeke kwenye chumba cha kuhifadhia pesa hizo na bwana Turma hakuwa na ubishi zaidi ya kuongoza hadi kwenye chumba wanacho hifadhia pesa pamoja na vito vya dhamani kama madini ya kila aina yenye dhamani kubwa sana katika mauzo yake.
Agnes akashusha mabegi makubwa matatu chini alilokuwa ameyabeba mgongoni na akayafungua na akaanza kazi ya kuviingiza vibunda vya pesa pamoja na vipande vya madini,begi lakwanza likajaa na akahamia kwenye begi jengine na kazi ikawa ndio hiyo hiyo ya kuweka pesa kwenye mabegi hadi mawili yakajaa babisa na jengine likafika nusu
“Anna take it”(ana chukua hilo)
Agnes akamsukumia Anna begi moja ambaye kwa wakati wote alikuwa amaishika bunduki yake kiumakini na kuielekezea kwa bwana Turma.Wakati ndani yakiendelea Alima,Rahab na Fety kazi yao ikwa nikuhakikisha hakuna kiumbe yoyote ambaye anaweza kujipenyeza na kufika katika eneo la nje ya banki.Gari tatu za watu binafi zilizo kuwa zinajaribu kukatisha katika eneo la karibu yao wakijifanya ni vichwa ngumu hawaelewi ni kitu gani kinacho endelea walizishambulia kwa risasi nyingi na kuwaua madereva pamoja na watu walimo ndani ya gari hizo
“R nenda kacheki ndani waambie waache pozi hapa nje hali ishakuwa tete”
    Fety alizungumza huku sura yake akiwa ameiziba na kofia maalumu ambalo limetobolewa sehemu za macho tuu na kofia lake linafanana na wezake wote waliomo ndani huku wakiwa wamevalia majaketi maalumu ya kuzuia risasi kupenya(bullet proof) huku suruali zao zikiwa ni nyeusi zenye mifuko mingi pamoja  na viatu vyeusi vya jeshi.
Rahab akaingia na kumuona askari mmoja akijaribu kunyata akielekea kwenye chumba cha kuhifadhia pesa huku akiwa na bunduki mkononi,Rahab hakufanya masihara zaidi ya kufyatua risasi zipatazo tato zilizo ukatisha uhai wa askari huyo na kumuangusha sakafuni kama mzigo na watu wengine wakavifunika vichwa vyao huku baadhi yao wakishindwa kuzizuia haja zao ndogo
Ikamlazimu Anna kuchungulia baada ya kusikia milio ya bunduki na kumuona Rahab akiwa anamgeuza geuza askari ailiye mpiga risasi kwa kutumia mguu kuhakikisha kama amefariki dunia au laa.
“Oya best fanyeni fasta tuibuke zetu hao machalii huko nje wamesha aanza kubweka kama bweha si munajua tena”
“Ndio tumemaliza njoo unyanyue hii ishu hapa”
Rahab akaingia na kuchukua begi lenye pesa nusu na kuliweka mgongoni na wakatoka wakiwa wameongozana huku kila mmoja akiwa ameishika bunduki yake vizuri
“Simameni juu wote”
Rahab alizungumza na kuwafanya wezake kushtuka
“Wewe unataka kufanya ishu gani tena twende zetu”
“Ngojeni musiwe na papara wanangu huko nje kimesha nuka na tukitoka hivi hatuwezi kufika mbali”
Wakamuacha Rahab afanye anacho taka kukifanya,Rahab akawaamrisha watu wote kuvua nguo zao hakujali kama kuna mkubwa au mdogo,msichana au mvulana wote jukumu lilikwa ni moja.Watu wote wakavua nguo zao zote na kubakiwa kama walivyo zaliwa na wote akawaamuru kufungua milango ya benki na kutoka nje na kukimbia la sivyo wote atawachakaza kwa risasi.
Alima na Fety wakashangaa kuona kundi kubwa la watu wakitoka wakiwa wapo uchi wakikimbia,Rahab,Anna na Agnes wakatoka wakijichanganya kwenye watu hao na Rahab akamrushia begi Fety na akaanza kuwashambulia askari ambao ndio wanasimamisha gari lao ili wapambane nao.
Rahab akaendelea kuwashambulia askari wapatao wanne na kuwafanya wapoteze maisha na wezake tayari walisha ingia ndani ya gari lao aina ya Rage rover,Idadi kubwa ya watu waliomo kwenye eneo hili wakaanza kutawanyika kila mmoja kuyanusuru maisha yake na kama mtu alihisi kama hayapendi maisha yake basi alijikuta akijerushiwa na wasichana hawa wenye roho za kikatili huku wakirusha mabomu ya machozi yapatayo kumi yaliyosababisha moshi mwingi katika eneo hili na watu wengi wakajikuta wakitokwa na machozi pasipo kupenda
Rahab akatupa bunduki yake na kuichomoa bastola yake na kujichanganya kwenye watu wanao kimbia kimbia wakiwa wamechanganyikiwa huku wezake wakiwasha gari lao na kutokomea wasipo pajua.
Dickson fundi maarufu wa baiskel eneo la benki ya biashara iliyo vamiwa na majambazi,naye akawa ni miongoni mwa watu walio jilaza ndani ya kiduka chake huku wakisubiria heka haka za majambazi kutoweka isitoshe moshi wa mabomu ya machozi ukiwaadhiri sana.Akastukia msichana akiingia ndani ya kiduka chake cha na kumuomba hifadhi ya muda,Dickson hakuweza kubisha kutokana na msichana huyo kushika bastola mkononi na kwa haraka akatambua ni miongoni mwa wale majambazi walio ivamia benki
“Ingia humo ndani”
Dickson akamuongoza Rahab kuingia ndani ya kijichumba anacho hifadhia spea mpya za baiskeli anazo ziagizia kutoka Zanzibar.
“Kaka ninakuomba usiseme chochote kwa mtu yoyote sawa”
“Sawa nimekuelewa”
Katika siku ambayo Polisi wanapata shida sana ni siku hii ambayo Benki ya CNB kuvamiwa na majambazi na kushindwa kumkamata jambazi hata mmoja na isitoshe wananchi wamedhalilishwa kwa kutembezwa uchi .Msako mkali ukaanza kufanyika katika jiji la Dar es Salaam na kila gari zinazo kwenda mikoani ni lazima zikaguliwe na kitu ambacho kinawaumiza akili askari ni kutoweza kuwafahamu majambazi hao japo kila wanapo wahoji hoji wahanga wa tukio hilo akiwemo meneja wa Benk ambaye muda wote analia kama mtoto mdogo anadai kuwa majambazi hao ni wasichana tena wanao onekana kuwa na umri wa miaka kati ya 21 hadi 25
“Huko nje vipi polisi wapo bado?”
Rahab alimuuliza Dikson ambaye anakazi ya kuchungulia nje kuangalia ni kitu gani ambacho kinaendelea
“Ndio wapo wanatoa toa maiti za watu walio kufa na kuweka mikanda ile ya njano”
“Ahaa powa”
Rahab akaanza kuvua nguo moja baada ya nyingine na kubakiwa na boxer na kumfanya Dikson kumshangaa jinsi uzuri wa Rahab ulivyo kwani ni mrefu kiasi,sura yake ndogo iliyo jengwa na macho malaini na mazuri ya kuvutia,pua ndogo iliyo chongoka kidogo na unaweza kusema ni jamii ya mabinti warembo wa kisomali,Wembamba wake unavigezo vya kumfanya kuwa miongoni mwa wasichana wanao stahili kugombania umisi Tanzania hata umisi wa Dunia.
Rangi yake ya mwili ya kahawia inazidi kuufanya mwili wake kuwa kivutio kizuri mbele ya macho ya Dikson na kumfanya abaki akiwa amemtizama kwa dakika kadhaa gafla akajikuta akitazamana na mdomo wa bastola iliyo shikwa na Rahab
“Usishangae sana kijana”
Rahab alizungumza huku akiishusha bastola yeke chini na kumafanya Dickson kuirudiasha sura yake kwenye tukio la askari wanaondelea kufanya mahojiano na watu walio kuwepo katika eneo hili.Dickson akamshuhudia bodo boda mmoja wa pikipiki akizungumza na askari wawili ambao akanyoosha kidole chake kilipo kiduka chake akiashiria kuna kitu wakakitazame ndani ya kiduka hiki na taratibu askari wakaanza kupiga hatua za kuelekea kwenye kaduka ka Dikson
“Shiiti polisi wanakuja huku”
“Wapo wangapi?”
“Wawili”
“Wameshika bunduki mkononi”
“Sasa wewe jikaushe na atakaye ingia humu ndani halali yangu”
“Mmm”
Tayari polisi wamesha fika nje ya duka la Dickson na kuanza kulitazama tazama kwa umakini

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top