Mtunzi: Enea Faidy
Ilipoishia sehemu ya tatu ( kama hukuisoma bofya hapa)
Dorice akamsogelea Doreen kwa hatua chache.
"Jana ulikuwa na nani pale kwenye mti usiku?" aliuliza Doreen huku akiuchezesha mguu wake wa kulia chini na mkono mmoja akiwa kaushika kiunoni.
"hukuniona au?" aliuliza Dorice kwa mshangao.
"jibu swali!"
"OK! nilikuwa na Eddy"
"nani yako Eddy?"
"Doreen unanitisha ujue?"
"kha! nakutisha nina mapembe hapa? nijibu swali langu"
"Eddy mpenzi wangu!"
"nimekupata sasa... tangu lini Eddy mpenzi wako hujui kama ni mume wangu mtarajiwa?"
"Ati nini....... Eddy ni. .."
"Jana ulikuwa na nani pale kwenye mti usiku?" aliuliza Doreen huku akiuchezesha mguu wake wa kulia chini na mkono mmoja akiwa kaushika kiunoni.
"hukuniona au?" aliuliza Dorice kwa mshangao.
"jibu swali!"
"OK! nilikuwa na Eddy"
"nani yako Eddy?"
"Doreen unanitisha ujue?"
"kha! nakutisha nina mapembe hapa? nijibu swali langu"
"Eddy mpenzi wangu!"
"nimekupata sasa... tangu lini Eddy mpenzi wako hujui kama ni mume wangu mtarajiwa?"
"Ati nini....... Eddy ni. .."
Sehemu ya nne
.... DORICE alishtuka sana kusikia Eddy ni mume mtarajiwa wa Doreen hakutaka kuyaamini maneno ya Doreen hata kidogo.
"hivi we Doreen umechanganyikiwa au upo timamu?" Dorice aliropoka kwa hasira.
"
nikuulize wewe, hivi upo timamu au mwendawazimu unavomng'ang'ania
mpenzi wangu Eddy? mpaka watu wanakushangaa! inaniuma sana Dorice usione
nimekukaushia!" Alisema Doreen kwa msisitizo wa hali ya juu. Maneno
ambayo yalizidi kumuumiza Dorice mpaka machozi yakaanza kumlengalenga
machoni mwake. Alimtazama Doreen kwa hasira huku akiumanisha meno yake
kwa ghadhabu, moyoni alitamani kumuadhibu vikali Doreen kwa kutaka
kulitia DOA penzi lake na Eddy lakini hakuwa na uwezo huo.
"Ama
kweli kikulacho ki nguoni mwako! sitaki kuamini kama rafiki yangu
kipenzi Leo unageuka adui yangu!"alisema Dorice huku akipiga hatua na
kutaka kuondoka mbele ya mbaya wake. Lakini ghafla Doreen akamvuta shati
na kumrudisha pale alipokuwa amesimama.
"we vipi? hebu niache niondoke?"
"nitakuachaje
sasa wakati unaniharibia penzi langu na Eddy?" alisema Doreen kwa
kujiamini sana huku akibetua midomo yake kwa dharau utadhani Eddy ni
mpenzi wake kweli kumbe hakuna lolote ni tamaa na wivu vinavyomsumbua.
"umefanikiwa
kuniumiza moyo wangu Doreen mpaka najuta kukufahamu.... haya Fanya
lolote utakalo tena ili kunyang'anya haki yangu ya mapenzi... do it!"
alisema Dorice kwa kwikwi kwani alishindwa kuzuia kilio chake kutokana
na maumivu makali aliyoyapata moyoni mwake kwani maneno ya Doreen
yalikuwa kama mkuki wenye sumu katikati ya moyo wake.
"hata Mimi najuta kukutana na mwanaharamu wewe, Kwa usalama wako achana na Eddy... sijui unanielewa?"
Dorice
hakusema chochote zaidi ya kumkazia macho ya hasira Doreen, bila kujua
kuwa kutazamana na Doreen kwa wakati ule ilikuwa ni kujikaanga kwa
mafuta yake mwenyewe kwani Doreen aliitumia nafasi ile vizuri sana.
Alijibadilisha
macho yakawa ya kutisha sana kisha kila alipomtazama Dorice machoni
alimhamishia vitu Fulani visivyoeleweka, kisha baada ya hapo Doreen
alimsogelea Dorice na kumzodoa lakini haikuwa kumzodoa kwa kawaida Bali
alimpaka vitu kama kamasi USO mzima na kumfanya Dorice atie kinyaa sana
bila yeye mwenyewe kujitambua.
"hebu
niondokee hapa mpuuzi wewe na ushukuru Mungu sijakufanya kitu kibaya"
alisema Doreen baada ya kuhakikisha amekamilisha kazi yake aliyokusudia
kwani sio siri Doreen alipania kumpata Eddy kwa vyovyote vile.
Dorice alitembea taratibu na kumfuata Eddy darasani huku akiendelea kulia.
**********
Walimu
wote walikuwa hawaelewi mambo yanayoendelea shuleni pale, kwani kila
siku liliibuka jipya. Suala la mwalimu John kuvuliwa suruali kwa
mazingira ya kutatanisha lilizidi kuwapa maswali mengi walimu wa while
ya sekondari mabango mpaka wakaogopa hata kuingia madarasani, kwani
walihisi wanaweza kudhalilishwa kama ilivyomtokea mwalimu John.
Mbali na suala hilo pia suala la mkuu wa shule kujifungia ofisini liliwapa mtihani mkubwa kwani haikuwa kawaida yake.
"jamani
nimeenda ofisi ya mkuu wa shule karibia Mara tatu nimegonga sana lakini
hakutoa jibu hata nilipojaribu kusukuma mlango inaonekana amefunga kwa
ndani!" alisema makamu mkuu wa shule baada ya kuingia staff.
"hata
Mimi nimeenda pale ofisini lakini palikuwa kimya sana ingawa mlango
unaonekana umefunguliwa kwa nje... nimepiga simu haipokelewi" alisema
mtaaluma.
kiukweli iliibuka sintofahamu miongoni mwa walimu wote waliingiwa na hofu kubwa.
" mmh! hii sio kawaida ya mkuu kabisa inabidi tufanye jambo"
"Mimi naona tuvunje mlango tu" alipendekeza mwalimu wa nidhamu.
walimu
wote walikubaliana kuvunja mlango wa ofisi ya mkuu wa shule. wakaebda
moja kwa moja mpaka ofisini kwa mkuu na kuvunja mlango kisha wakaingia..
walichokutana nacho kila MTU hakuamini , walibaki midomo wazi huku
machozi yakiwadondoka kama chemichemi katikati ya mlima.
Mwili
wa mwalimu Mbeshi ulikuwa umeoza vibaya sana funza walitapakaa kila
mahali wakisindikizwa na harufu mbaya iliyojaa ofisini mle. hakuwa
mbeshi tena mwanamama aliyejipenda na kunukia marashi muda wote Bali
jina lilibadilika na kuwa maiti.
Walimu
walitulia kimya kwa muda wa dakika mbili nzima Vila kusema chochote
lakini macho ya makamu mkuu wa shule yalitua mpaka mezani kwa mbeshi
ambapo aliona karatasi ndogo nyeupe yenye ujumbe. Akaisogelea na
kuichukua, kisha akaanza kuisoma. Ghafla alishtuka sana baada ya kusoma
ujumbe ule "UNAFATA WEWE ULIYESOMA KARATASI HII."
Makamu
yule kwa woga na hamaki akaropoka " Mimi sijasoma chochote...
tusisingiziane hapa!" alisema huku akificha macho yake na kumkabidhi
mtaaluma karatasi ile kwani walimu wote hawakujua kilichotokea hivyo
wakatamani wasome ujumbe uliokuwemo mle.
********
Dorice alimtuma MTU amwitie Eddy darasani lakini mwanafunzi yule akakataa. hivyo Doreen aliamua kwenda mwenyewe darasani mle.
Darasa
lilikuwa limetulia kimya sana, Dorice akafungua mlango na kuingia
lakini ghafla alipoingia wanafunzi wote darasani mle wakacheka kicheko
kikali sana kilichomtia hofu sana Dorice. lakini akajikaza kisabuni
licha ya kwamba alijua wanamcheka yeye, akamsogelea Eddy na kumtaka
watoke nje lakini Dorice aligundua mabadiliko makubwa sana kwa Eddy Ila
hakuuliza chochote wakatoka nje. wanafunzi wakacheka tena kwa dharau
kitendo kilichomuumiza sana Dorice.
"hivi we demu unajisoma??" alisema Eddy kwa ukali. maneno hayo yalimshtua sana Dorice.
"Eddy! sijakuelewa!"
" unajisoma kweli? hivi kwanza unajua majamaa wanakucheka kwa sababu gani?" maneno ya Eddy yalimfanya Dorice ataharuki.....
Post a Comment Blogger Facebook