0

Maisha ni safari na hatutakiwi kukata tamaa kwa kuwa hatujui kesho yetu. Ukiisikia historia ya maisha ya mchekeshaji ambaye kwa sasa amegeuka kuwa mtangazaji wa Clouds FM, Kicheko unaweza kutokwa na machozi kama huna uvumilivu.


Awali Kicheko alikuwa member wa Ze Comedy ya EATV baada ya kuchaguliwa kwenye shindano la kutafuta wasanii watakaogiza kwenye kipindi hicho ambapo alidumu hapo kwa muda wa miaka isiyopungua miwili.

Waswahili wanasema “acha kazi, uone kazi, kupata kazi, ilivyokuwa kazi,” lakini kwa Kicheko haikuwa ngumu kwake kuacha kazi EATV ya uchekeshaji baada ya kuchukua maamuzi ya kuandika barua ya kuacha kazi kwenye uongozi wa kampuni hiyo April, 2014 huku akiwa hana kazi. Lakini pia mtangazaji huyo amepinga taarifa za kuwa alifukuzwa kazi kwenye kituo hicho cha runinga.

Baada ya muda kupita Kicheko alifanikiwa kupata shavu la utangazaji kwenye redio ya EFM akiendesha kipindi cha Singeli ‘Genge’ ambacho kimekuwa kikipendwa zaidi na mashabiki mitaani na kufanya brand yake kuanza kuwa kubwa.

Kumbe ilikuwa ni dhahabu huku wengi wakidhani lilikuwa ni jiwe, rangi yake ilifichwa na vumbi ndiyo maana kila mpita njia alilidharau kabla ya EFM na hatimaye Clouds FM kuliokota jiwe hilo na kulisafisha na hatimaye sasa rangi yake halisi imeonekana na kila mtu ameanza kulitamani tena.

Akikaribishwa kwa mara ya kwanza leo kwenye ofisi za Clouds Media (mjengoni) kwenye kipindi cha ‘Leo Tena’ mtangazaji huyo ameelezea historia yake kidogo huku akidai kuwa aliwahi kuwa mwizi huko nyuma. “Mwanzo nilikuwa mwizi, mkabaji. Unajua haya ni maisha tu,” amesema Kicheko.

Kwa sasa Kicheko amepewa heshima kubwa na watu wa mtaani ikiwa ni pamoja na kumpa jina la ‘Rais wa Uswazi’ kutokana na support yake anayoitoa kwenye muziki wa Singeli ambao umeonekana kukubalika zaidi kwa sasa huku akiwa na wanachama 489 kwenye kikundi chake.

Mchekeshaji huyo anatarajiwa kuanza kazi kwenye kipindi kipya kiitwacho ‘Uswazi Flava’ hapo Clouds FM.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top