Katika
hali isiyokuwa ya kawaida Prof Lipumba ameendelea Kung’ang’ania kiti
cha uenyekiti wa chama chake cha CUF na kusema kikao kilichokaa jana
visiwani Zanzibar na kufanya maamuzi ya kuwasimamisha uanachama,
hakikuwa halali na kilikuwa nje ya katiba ya CUF, sababu mojawapo ikiwa
ni kuwekwa kando kwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya.
“Kikao
hicho hakikuwa halali, haiwezekani Baraza Kuu linakaa halafu Naibu
Katibu Mkuu Bara hajui, wala hakujulishwa, na bado kuna wajumbe wengine
hawakuhusishwa” Alisema Prof Lipumba
Lipumba
aliongeza kuwa ni kweli alijiuzulu uenyekiti, lakini baadaye aliamua
kuandika barua kwa Katibu Mkuu ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu na
sasa yeye ndiye Mwenyekiti halali wa chama hicho.
“Nilimuandikia
barua ya kurudi kwenye nafasi yangu, akasema anasubiri ushauri wa
kisheria, lakini hadi sasa hakuna kitu, hiyo inamaanisha kuwa sasa mimi
naendelea na nafasi yangu, na niko ngangari kama mwenyekiti” Alisema Prof Lipumba.
Aidha aliongeza kuwa alitaka kujieleza katika mkutano mkuu mbele ya wanachama, lakini mkutano ule ukavurugwa.
Kuhusu
kuwepo kwa tofauti kati yake na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif
Sharif Hamad, Prof Lipumba amesema kuwa huenda kuna tofauti kwa kuwa
mara nyingi huwa hamuelewi jinsi anavyokiendesha chama bila kifuata
misingi ya kidemokrasia.
“Katibu
Mkuu anamdharau na hampi heshima yake Naibu Katibu Mkuu Bara, mara
nyingi huamua mambo yake bila kushirikisha viongozi wengine, halafu sasa
anataka kufukuza wanachama, huwezi kuwa na chama halafu ufukuze
wanachama, wanachama wanatafutwa duniani kote, halafu wewe unawafukuza,
hizo ni dalili za uongozi wa kiimla, kuongoza chama unapaswa kujali
demokrasia na siyo kuwa dikteta ndani ya chama” Amesema
Kuhusu
Julius Mtatiro kuwa mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uongozi, Lipumba
amesema kuwa hatambui maamuzi hayo, na wala hamtambui Mtatiro kama
kiongozi wa chama hicho bali mjumbe wa Mkutano Mkuu, nafasi ambayo yeye
ndiye aliyempa.
“Mtatiro
hawezi kuwa mwenyekiti, mimi ndiye mwenyekiti wa chama, Mtatiro
alishindwa hata kuongoza mkutano mkuu, ukavurugika, hawezi, simtambui”
Post a Comment Blogger Facebook