ZOTEHAPA BLOG

Wednesday, February 3, 2016

Gari la CRDB laopolewa, mfanyakazi hajapatikana


 Gari hilo liliopolewa jana saa nane mchana baada ya kulitafuta kwa siku tano tangu lilipozama Mto Kilombero Januari 27 likiwa katika kivuko cha MV Kilombero II.
Kilombero. Gari la Benki ya CRDB limeopolewa katika Mto Kilombero likiwa na Sh3.5 milioni, huku mfanyakazi wake akiwa hajapatikana.

Gari hilo liliopolewa jana saa nane mchana baada ya kulitafuta kwa siku tano tangu lilipozama Mto Kilombero Januari 27 likiwa katika kivuko cha MV Kilombero II.

Mfanyakazi wa CRDB tawi la Ifakara, Dustan Rwegasira (31) ni miongoni mwa abiria waliokuwamo ndani ya kivuko hicho.

Hata hivyo, jitihada mbalimbali za kukiibua kivuko hicho bado zinaendelea baada ya juzi kutumia mbinu ya kutumbukiza mapipa yaliyojazwa maji kisha kuzamishwa chini ili kukitoa kukwama.

Kazi hiyo inafanywa na timu ya wazamiaji wa Kampuni za M.Divers Limited na May-Marine Go Limited.

Mkuu wa Kikosi cha Uzamiaji na Uokoaji wa Kampuni ya M. Divers Limited, Hafidh Seif alisema: “Hesabu zetu zinakwenda vizuri, yale matangi unayoyaona yanazamishwa baada ya kujazwa maji halafu, yakiwa chini yatageuka maboya kisha yatapanda juu na kivuko hicho na kuvutwa na wenye magari,” alisema Seif.

Seif alisema wanakabiliana na changamoto ya kasi ya maji, lakini wanamshukuru Mungu kazi ya kuondoa maji ndani ya vyumba vya maboya ya kivuko imemalizika salama. 


Posted by Unknown at 4:55:00 AM
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Labels: KITAIFA

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Post Labels

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
.disqus.com/recent_comments_widget.js?num_items=4&avatar_size=32&excerpt_length=100&hide_mods=0">

Labels

Breaking News

Main Menu

Top Menu

Contact us

Name

Email *

Message *

twitter

Tweets by @zotehapa1

facebook

Zotehapa1

mapenzi na simulizi

Popular Posts

  • Usher - No Limit ft. Young Thug
  • Mbunge wa Tarime John Heche Ashawishi Bunge Kuridhia Posho za Kikao cha leo Zipelekwe Kwa Wahanga wa Tetemeko
    Mbunge wa Tarime John Heche (UKAWA-Chadema) amefanikiwa kulishawishi bunge kuridhia posho za leo tarehe 13 za wabunge zipelekw...
  • Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi siku 23 tangu amteue
  • JIMAMA MTAA WA PILI (sehemu ya 17)
    ILIPOISHIA..……. Ghafla tulisikia mlango unagongwa, “kuna mtu!” Fridah aliongea kwa sauti, huku mimi nikiendelea kupiga mikiki. ...
  • MH ZITTO KABWE ATAJA ORODHA YA WENYE PESA SIZIZO HALALI KWENYE BENKI YA HSBC USWISI
           M h Zitto Kabwe akihutubia wananchi wa mwembeyangajijini Dar es salaam aliyasema haya. Kwanza nianze kwa kutoa shukran kwa kuitik...
  • Mbowe Aanza Kulisuka Baraka Kivuli La Mawaziri
    Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametoa mwelekeo wa upangaji wa uongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni na baraza kivuli la mawaziri...
  • Manchester United striker Robin van Persie has undergone a medical with Turkish club Fenerbahce and has agreed to join on a three-year contract, according to various reports.
    ​ ​Sky Sports announced that a deal between the two clubs had been struck on Wednesday night, after Fenerbahce director Guiliano Terraneo...
  • Mbowe asakwa na polisi, hiki ndicho alichoandika
  • Kanisa Katoliki Laja na Mpya..Sasa Kama Upo Kwenye Ndoa Unaweza Mpa Mwenzako Talaka..Kama Wafanyavyo Waislam
    KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis jana alieleza mabadiliko mapya yanayolenga kuwarahisishia Wakatoliki kuvunja ndoa zao...
  • Mwimbaji Ruby Akimbilia EFM Radio Baada ya Ugomvi wa Maslahi Kati ya Mwimbaji Huyo na Clouds FM
    Pichani Ruby akiwa Kwenye Tamasha la EFM Mwimbaji Ruby ambae alikuzwa na kulelewa na Clouds FM Baada ya Kufanya vizuri katika mashin...

About us

ads

youtube

ads

UDAKU

Awesome Inc. theme. Powered by Blogger.