watu wasiojulikana wamevamia na kuvunja ofisi ya kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuiba kompyuta na vifaa vingine.
Habari tulizozipata ambazo zimethibitishwa na Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam zinasema miongoni mwa kompyuta zilizoibiwa ni ile iliyokuwa inatumiwa na Dr Philip Mpango alipokaimu nafasi ya Kamishna mkuu wa TRA kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha
Kwa mujibu wa chanzo hicho,huenda kompyuta hiyo ikawa na taarifa muhimu kuhusu ukwepaji wa kodi na sakata la makontena Bandarini.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Ya Dar es salaam,Simon Sirro amesema tayari jeshi hilo linawashikilia watu wanne kwa uchunguzi zaidi
Siro alitaja vitu vilivyoibwa katika ofisi hiyo kuwa ni Kompyuta mbili, Televisheni moja na King'amuzi.
Alisema wanaoshikiliwa ni walinzi wawili kutoka kampuni ya Suma JKT ambao walikuwa zamu usiku huo, Katibu Muhtasi pamoja na Karani wa Ofisi hiyo.

Post a Comment Blogger Facebook