Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2015/2016 inatazamiwa kuanza
kutimua vumbi jumamosi Septemba 12, 2015 kwa michezo saba kuchezwa
katika viwanja tofauti nchini.
Ndanda
FC ya Mtwara watakua wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa
Nagwanda Sijaona mjini Mtwara, Wana kimanumanu African Sports
watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku
Wana Lizombe Majimaji wakiwa wenyeji wa maafande wa JKT Ruvu katika
uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Azam
FC watakua wenyeji wa Tanzania Prisons kaika uwanja wa Chamazi Complex,
Stand United FC chama la wana watawakaribisha Mtibwa Sugar katika
uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Toto Africans watawakaribisha
Mwadui FC uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya City watacheza na Kagera Sugar
katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Jumapili
Ligi Kuu itaendelea kwa mchezo mmoja tu utakaochezwa katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam ambapo mabingwa watetezi wa kombe hilo Yanga
SC watawakribisha wagosi wa kaya Coastal Union.
Katika
hatua nyingine klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera itatumia Uwanja
wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kwa mechi zake za nyumbani dhidi ya
Toto Africans (Sept 26), JKT Ruvu (Sept 30), Tanzania Prisons (Oct 4) na
Yanga (Oct 31).
Mabadiliko
hayo yamefanyika kupisha shughuli ya uwekaji nyasi bandia inayoendelea
kwenye uwanja wao wa Kaitaba mjini Bukoba unaofanywa na wataalamu kutoka
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Post a Comment Blogger Facebook