
CONFESSION! Msanii wa filamu Bongo, Diana Kimari ameanika ukweli wa
moyoni kuwa, alianza kujihusisha na mambo ya mapenzi akiwa anasoma shule
ya msingi.
Akipiga stori na Amani, Diana alisema alianza kuwa na uhusiano wa
kimapenzi akiwa darasa la saba na hii ni baada ya kuingia kwenye utu
uzima ‘kuvunja ungo’ kitu ambacho huona kwamba zile zilikuwa akili za
kitoto na kwamba hakukuwa na ‘ladha ya mapenzi’ hivyo huwa hataki
kukumbuka kabisa nyakati hizo

“Ni kweli mimi si mgeni wa mapenzi, niliwahi kuwa na mpenzi tangu nikiwa
shule ya msingi, japo hayakuwa na ladha maana si unajua mapenzi ya
utotoni tena? Kwa sasa sina tena hamu na wanaume, nimeshaumizwa sana na
mapenzi, sasa mimi na shule tu,” alisema Diana anayesomea biashara
katika chuo kimoja kilichoko mkoani Kilimanjaro.
Chanzo: GPL
Post a Comment Blogger Facebook