Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na
bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa (pichani) amesema kikosi chake kipo
tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali
za Mataifa ya Afrika mwaka 2017.Akiongea na waandishi wa habari leokatika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume, Mkwasa amesema vijana
wake wapo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo huo wa kesho ambao ni
muhimu kwa Taifa Stars.“Tumefanya mazoezi kwa takribani siku kumi,
vijana wako katika hali nzuri ya mchezo, uwezo waanaouonyesha mazoezini
ni wa hali ya juu na unatupa matumaini ya kufanya vizuri” Alisema
Mkwasa.Aidha Mkwasa amesema katika mpira hakuna kinachoshindakana,
anatambua Nigeria ni timu kubwa Afrika, wameshatwaa ubingwa wa Afrika
mara tatu, lakini mpira wa sasa lolote linaweza kutokea, hivyo sisi
tumejiandaa vilivyo kufanya vizuri katika mchezo huo.Mwisho Mkwasa
amesema wamejindaa vizuri kwa mchezo huo wa kesho, na kuwaomba
watanzania kuja kuwapa sapoti wachezaji uwanjani kwa kuwashangilia muda
wote wa mchezo, na kusema kikosi chake hakina mchezaji majeruhi hata
mmoja kuelekea kwa mechi hiyo.Mechi hiyo ya kesho jumamosi itachezeshwa
na waamuzi kutoka nchini Rwanda ambao ni Louis Hakizimana (mwamuzi wa
kati) Honore Simba (mwamuzi msaidizi), Jean Bosco Niyitegeka (mwamuzi
msaidizi), Abdoul Karim Twagiramukiza (mwamuzi wa akiba) na kamisaaa wa
mchezo ni Charles Kasembe kutoka nchini Uganda ambao wote tayari
wameshawaili jijini Dar es salaam tangu jana jioni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
.disqus.com/recent_comments_widget.js?num_items=4&avatar_size=32&excerpt_length=100&hide_mods=0">
Post a Comment Blogger Facebook