Dar
es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania leo imetoa hukumu yake na kulipa
ushindi gazeti la Mwanahalisi baada ya mahakama hiyo kujiridhisha kuwa
Waziri wa Habari na Utamaduni, Dk Fenella Mukangara hakufuata taratibu
la kukifungia chombo hicho cha habari.
Gazeti
la Mwanahalisi lilifungiwa Julai 30, 2012 kwa amri ya Dk Mukangara kwa
kutumia mamlaka aliyopewa na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.
Akitangaza
kulifungia gazeti hilo mwaka 2012, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(Maelezo), Fabian Rugaimukamu alisema kuwa gazeti hilo limefungiwa kwa
sababu limekuwa na mwenendo wa kuandika habari na makala za uchochezi na
zinazojenga hofu kwa wananchi.
Wakili
wa Kampuni ya Hali Halisi Publisher , Rugemaleza Mashamala amesema
ingawa hawajapewa hukumu mkononi lakini kutokana na ushindi waliopewa
na mahakama ni halali na wana haki ya kuendelea na uchapishaji.
Hata
hivyo alisema ni lazima upande wa serikali waone uamuzi wa kimaandishi
uliotolewa ili kujiridhisha na kuendelea na taratibu nyingine.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
Post a Comment Blogger Facebook