BAADA ya timu ya vijana ya Stand United kupokea
kipigo cha mabao 4-0 juzi Jumapili, imebainika kwamba Kocha Mkuu wa
klabu hiyo, Mfaransa Patrick Liewig amegoma kupeleka kikosi cha wakubwa
kushiriki michuano maalumu kwa timu za Kanda ya Ziwa zinazocheza Ligi
Kuu Bara.
Mfaransa huyo ameuambia uongozi kwamba bado kikosi
chake hakijajengeka kwa mashindano hivyo kugoma kuipeleka timu kupata
aibu na badala yake jukumu hilo akaliacha kwa timu ya vijana chini ya
miaka 20 ya Stand.
Kikosi hicho cha U-20 cha Stand kilikutana na
dhahama ya kufumuliwa na Mwadui FC iliyo chini ya kocha Jamhuri Kihwelo
‘Julio’ katika mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga.
Ofisa Habari wa Stand United, Deo Makomba,
ameliambia Mwanaspoti kuwa Liewig ametoa programu yake kuwa ataanza
kucheza mechi za kirafiki baada ya siku kumi tangu timu hiyo ilipoingia
kambini juzi Jumapili katika mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama mkoani humo.
“Tunaheshimu mashindano hayo ila kocha amesema
kuwa bado anatengeneza kikosi hivyo asingeweza kuipeleka timu ya wakubwa
kwenye mashindano hayo,” alisema Makomba.
Post a Comment Blogger Facebook