Marafiki wa Wafanye Watabasamu, hivi karibuni, walitembelea kituo cha watoto yatima (Amani Orphanage Centre) kilicho katika Kijiji cha Zinga, Bagamoyo kwa ajili ya kutoa misaada mbali mbali kisha kuchora nao. Mbali na marafiki waishio nchini, pia kulikuwa na walimu sita toka Shule ya Msingi ya Catton Grove ya Uingereza na wawakilishi wa taasisi ya The Tanzania Norwich Association pia ya Uingereza. (Picha: Nicolas Calvin).
Msafara wa Wafanye Watabasamu ukiwasili kituoni hapo. Zaidi kuhusu programu hii tembelea:https://www.facebook.com/wafanyewatabasamu.
Mkurugenzi wa kituo cha Amani Orphanage Centre, Bi. Margareth Mwegalawa wa pili toka kulia aliyesimama, akitoa taarifa fupi kuhusu kituo hiko.
Mratibu wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni mchora vibonzo ITV, Nathan Mpangala akiwashukuru marafiki mbalimbali waliochangia misaada na kufanikisha ziara hiyo.
Sanaa ya uchoraji nayo ikachukua nafasi yake.
Mmoja wa watoto wa kituo hiko akijitambulisha kwa wageni.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hiko wakifurahi na wageni waliowatembelea. Kituo hiko kina watoto 37.
Watoto wa Kituo cha Amani Orphanage Centre walimwaga shoo ya nguvu kwa wageni.
Baadhi ya marafiki wa Wafanye Watabasamu wakijiachia na watoto.
Baadhi ya watoto na marafiki wa Wafanye Watabasamu wakionesha kazi zao.
Naam, raha ya shughuli mlo bwana.
Post a Comment Blogger Facebook