0
Ni mwaka wa Uchaguzi Tanzania ambapo upinzani mkubwa unaonekana kwenye Wagombea wawili ambao ni John Pombe Magufuli atakaegombea kupitia CCM na Edward Lowassa aliyechukua fomu ya CHADEMA kwenye headlines za muungano wa vyama vya upinzani (UKAWA)

Tayari mpaka sasa tumeona baadhi ya mastaa wa Tanzania wakiweka wazi watu wanaowakubali kati ya hawa wawili, miongoni mwao ni Wema Sepetu aliyeweka wazi kumsupport Magufuli, mwigizaji Jackline Wolper na Aunty Ezekiel wanamsupport Edward Lowassa na sasa ni Diamond kaweka wazi.

Diamond anamsupport John Pombe Magufuli na kayaandika haya >>> Iwe Msanii, Mtangazaji, ama Mwanamichezo, ila Kila Mtanzania anahaki ya Kuchagua kiongozi anaeamini ni Bora, Mchapa kazi, Mwenye Afya na Msimamo ili kutuendelezea Nchi yetu… Kwa Uchunguzi na tathmini niliyoifanya tangu hizi mambo za Kampeni zianze nimegundua na kuamini kuwa huyu ndio Jembe’


Kwenye sentensi ya pili Diamond akaandika >>> ‘Nitakuandikia na kukupostia ushahidi kukuthibitishia kwanini nimeona John Magufuli Pombe ndie anaefaa… unapohisi na wewe una fact za kumtetea umtakaye karibu uniambie hapo halaf na mi nikumwagie zangu, ila usijisumbue Matusi coz hayatokusaidia wala kunisaidia kunibadilisha akili yangu kwa sababu sanasana ntakuona Huna akili Maana nishayazoea, nipe fact zako nami nikupe zangu ili pamoja Tujenge nchi….. #HapaKaziTu #Ccm

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top