Klabu ya soka ya Athletic Bilbao
imetwaa ubigwa wa kombe la Super Cup nchini Hispania baada ya kwenda
sare ya kufunga bao 1-1 na Barcelona.
Bilbao wametwaa ubingwa huo
baada ya miaka 31 katika mchezo ulichezwa katika dimba la Nou
Camp.Katika mchezo wa fainali ya kwanza uliochezwa kwenye dimba la San
Mames Bilbao walipata ushindi wa mabao 4-0.Mshambuliaji Lionel Messi ndio alianza kuiandikia timu yake bao dakika 44 kabla ya Aritz Aduriz kuisawazishia timu yake katika dakika ya 81 ya mchezo na na kuihakikishia ubingwa huo kwa jumla ya mabao 5-1.
Beki wa Barca Gerard Pique na Kike Sola wa Bilbao walipewa kadi nyekundu katika mchezo huo.
Post a Comment Blogger Facebook