Kampuni ya simu Tanzania ambalo ni shilika kongwe la umma(TTCL)asa imefilisika kibiashara kutokana na ubia tata kati ya serikali na wawekezaji wenye mgongano wa kimaslahi katika sekta ya mawasiliano.
Aidha, ubovu wa menejimenti, ubadhirifu wa fedha za umma, wafanyakazi waliokatishwa tamaa, ukosefu wa mtaji, madeni sugu, na mitambo iliyopitwa na wakati ndivyo vinavyochangia kuliua.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa
TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura, kampuni hii inachungulia kaburi kwa sababu
imekuwa ikipata hasara mwaka hata mwaka kiasi cha kufikia hadhi ya
“kutokopesheka.
Kwa mujibu wa Dk. Kazaura, “kwa sasa
Kampuni ya TTCL ni mufilisi,” hatua ambayo inatokana na “mbia mwenye
hisa za asilimia 35, kutofanya uwekezaji mkubwa tangu aingie katika ubia
na serikali mwaka 2001.”
Dk. Kazaura aliyasema hayo mjini Dodoma mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi.
Nae Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, amesema mchakato wa kuondoka kwa
Kampuni ya Airtel kutoka TTCL “uko katika hatua za mwisho.” Ameeleza
kuwa tayari “makubaliano ya bei” ya hisa zinazodaiwa kumilikiwa na
Airtel katika TTCL yamefikiwa “katika kikao cha majadiliano
kilichofanyika tarehe 20 Novemba 2014.“
Akielezea majadiliano yalivyokuwa, Profesa. Mbarawa amesema Kampuni ya Airtel “iliafiki
kuachia hisa inazomiliki ndani ya TTCL” na kisha Serikali kukubali
“kuzinunua hisa hizo kwa Sh. bilioni 14.9″ za Tanzania.
Tayari “Baraza la Mawaziri liliidhinisha
Serikali kununua hisa hizo” kwa mashrati kwamba malipo hayo yafanywe
“baada ya taratibu za kisheria kukamilika” ili hatimaye “Serikali iweze
kuimiliki TTCL kwa asilimia 100,” aliongeza Profesa Mbarawa.
Kufuatia kuibuka kwa taarifa za malipo haya, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kupitia kwa msemaji wake wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, (CUF) Mohamed Habib Mnyaa, imehoji umakini wa serikali na kuitaka itekeleze mambo kadhaa.
· Kwanza,
serikali imetakiwa kufafanua matakwa ya mkataba wa awali kati ya
Serikali na Kampuni ya MSI na hatua za utekelezaji wa makubaliano ya
mkataba huo mpaka sasa.
· Kueleza
iwapo mkataba huo ulikuwa unairuhusu kampuni ya MSI kuuza hisa zake kwa
makampuni mengine yaliyofuata kama vile Celtel, Zain na sasa Airtel.
· Kutoa ufafanuzi kuhusu uhalali wa maamuzi yake ya kuilipa kampuni ya Airtel Sh. 14 bilioni.
Post a Comment Blogger Facebook