Showing posts with label fasheni. Show all posts
Showing posts with label fasheni. Show all posts

Friday, March 4, 2016

Waziri Wa Maliasili Awasimamisha Kazi Watumishi 5 ,Wengine 15 Wahamishwa mamlaka ya Ngorongoro.

Waziri wa Maliasili na Utalii  Mh.Profesa Jumanne Maghembe amewasimamisha kazi watumishi watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuwahamisha wengine 15 kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha na ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa Umma.
Mh.waziri Maghembe amechukua hatua hiyo baada ya  kutembelea na kukutana na wafanyakazi wa mamlaka hiyo,na amese mahatua zingine zitafuata kwa watumishi hao ambao wote watano ni wa idara yauhasibu. Kuhusu  watumishi wanaohamishwa ambao ni wa idara mbalimbali ikiwemo uhandisi,utalii na ikolojia Mh.Prf.Maghembe amesema hatua hiyo inalenga kutoa mafasi ya kuendelea  kufanyika kwa uchunguzi zaidi juu ya tuhuma mbali mbali zinazowakabili. Mhifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro Bw.Fredy Manongi pamoja na kukiri kuwa mamlaka inakabiliwa na changamoto mbalimbali amesema kwa sasa tatizo kubwa ni ujangili unaofanyika katika maeneo ya mipakani japo amesema wanaendelea kuzikabili.  Hii ni ziara ya kwanza ya Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe katika mamlaka hiyo ambayo amesema ni mwendeleza wa utekelezaji wa azma ya serikali ya kuimarisha uwajibikaji,ukusanyaji wa mapato na kuimarisha  shughuli za uhifadhi.

Friday, January 22, 2016

UKAWA Walianzisha Tena Bungeni Wagomea Kamati za Bunge na Kususia Uchaguzi

Wakati vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vikitarajiwa kuanza leo kwa uteuzi wa wajumbe, wabunge wa upinzani tayari wameanza kwa kumtikisa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai, baada ya kususia uchaguzi wa wenyeviti wa kamati hizo.

Dalili za mgawanyiko kwenye kamati hizo zilianza kuonekana juzi, baada ya wabunge hao wa Kambi ya Upinzani kufanya kikao na kuweka msimamo wa kutaka kushirikishwa kwenye uteuzi wa wajumbe.

Kambi ya Upinzani ilisema inataka kushirikishwa katika hatua hiyo ikidai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM), imekuwa ikiwapangia watu wa kuongoza kamati zinazosimamia mapato ya serikali ambazo kikanuni zipo chini yao.

Viongozi hao wa kambi ya upinzani walidai kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakipangiwa watu wa kuongoza Kamati ya Hesabu za Serikali za (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ambazo kikanuni zinatakiwa kuongozwa na upinzani.

Baada ya Ofisi ya Bunge kutangaza majina ya wajumbe wa kamati, Kambi ya Upinzani Bungeni ilikutana na waandishi wa habari, lakini wakaahirisha kwa madai kuwa wamegundua kwamba orodha ya majina yaliyotoka, yana matatizo mengi zaidi.

  • “Tumegundua kwamba matatizo hayapo kwenye kamati ya PAC na LAAC tu, kwenye kamati nyingi kuna matatizo kwa hiyo kwa sasa viongozi wa kambi wanakutana kujadili na kuchambua taarifa iliyotolewa baadaye tutakutana na wabunge wote kisha kesho tutatoa msimamo wetu,” alisema Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, John Mnyika.


Baada ya kauli hiyo, Mnyika aliulizwa inakuwaje wao wanaendelea na vikao wakati wenzao wa CCM wakiwa kwenye uchaguzi:


  • “Siwezi kujibu chochote, neno lolote nitakalosema, nitaingilia hicho kinachojadiliwa na viongozi. Wewe subiri kwanza tumalize kikao, tutoke na msimamo wa pamoja na kesho tutawaeleza msimamo wetu,” alisema Mnyika.


Awali, kabla ya kutolewa kwa majina hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya, alisema kwa muda sasa wamekuwa wakichaguliwa watu wa kuongoza kamati hizo na CCM

  • “Ni sawa na mtu anakupa kitu kwa mkono wa kushoto na kukunyang'anya kwa mkono wa kulia. Ndiyo maana tukataka tushirikishwe kuanzia wajumbe watakaokuwa kwenye kamati hizo,” alisema Sakaya ambaye ni Mbunge wa Kaliua mkoani Tabora.


Kanuni za Kudumu za  Bunge Toleo la Aprili 2013, inasema: “Wenyeviti wa Kamati za Bunge zinazosimamia matumizi ya fedha za Umma ambazo ni Kamati ya Hesabu za Serikali, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, watachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe wa kamati hizo ambao wanatoka katika Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.”

Sunday, August 16, 2015

Namna yakujiweka fiti mda wote kwa mwanamke


Katika kujiweka fiti au tuseme kujiweka sawa kwa ajili ya kuonekana mrembo ni kazi ambayo inahitaji muda na uvumilivu vinginevyo unaweza kuwa sawa na chizi yoyote aliyejiwekea si tu maleba bali na mwili usiotamanika. 

 Na kwa mwanamke ambaye ana mji wake, watoto , familia na kazi inayohitaji ukakamavu mkubwa huku akitakiwa kuonekana bomba namchangamfu ni dhahiri kuwa la ziada lazima lifanyike vinginevyo mahali fulani utapwaya.unaweza kupwaya ofisini, ukaonekana huna maana , unaweza kupwaya nyumbani mtoto mkubwa akashindwa kukuangalia mara mbili na unaweza kupwaya mtaani watu wakajiuliza hee mama fulani vipi mbona usafi unamshinda?ndio kusema katika hili unahitaji mwanamke kuwa makini sana. Inavyoonekana wanawake wengi wanapokuwa katika mtawanyiko wa mambo hujisahau kabisa na mara nyingi husahau kabisa kuwa wanahitaji kula nakufanya vitu fulani ili kujiweka fiti.Kimsingi wanawake wote wawe wanachapa kazi kama wazimu, wawe na familia, wawe na mtoto mkubwa wanatakiwa kujiweka safi na sawa muda wote pamoja na majukumu yao yaliyotawanyika. 
 1) suiku zote hakikisha una tunda wakati wa kifungua kinywa chako. Hiiinasaidia kuondoa sumu katika mwili wako na kusaidia kuondoa uchafuuliojiweka kwa namna inavyostahili. 
 2) Kunyw amaji ya kutosha , punguza chai na kahawa kufikia angalauvikombe viwiuli kwa siku na muda uliobaki kunywa vinywaji ambavyo nivya mizizi kama jasmine, chamoile tea. Vinywaji hivi katika mfumoi wajuisi ni dawa tosha kwa ngozi yako na ili ionekane ya ujana muda wotena isiwe kavu.
 3) Huku umri wako ukiwa unapanda,punguza vyakula vya nafaka na kulazaidi matunda na mbogamboga ili kupunguza uzito.
 4) hakikisha unatembea vya kutosha na kujinyoosha ili uwe na mwili wakuvutia, mwembamba na wenye nguvu za kutosha na wa ujana.
 5) Punguza uvutaji sigara na pombe kwani ni vitu viwili vinavyozeeshangozi kwa kasi.
 6) Ongeza vyakula vya samaki katika chakula chako au aina yake
 7) Uwe unakula na mizizi inayokabiliana na uzee kama tulsi, amla, ashwagandha 
 8) Jipatie vitamu vya asili kama asali na raisins. 
 9) Kula vyakula vyako unavyopenda vya hovyo angalau mara moja kwa wiki 
 10) Kujisikia vyema ni namna bora za kukufanya uwe mwanamke bomba naanayevutia muda wote. 
 NB:Kujisikia vyema huku ni kujipenda mwenyewe kama hujipendi huwezi kuvutia na kama unaridhika kwa sababu ya kuridhika una tatizo kwelikwel

Post Labels