Mtunzi: Enea Faidy
.....DOREEN
alimkubalia Eddy kuwa mpenzi wake lakini alimweleza kuwa kuna sharti
ambalo Eddy lazima alifuate ndipo awe nae.Dorice hakutaka kukubali
kirahisi kumwachia Doreen kuwa na Eddy hivyo alipanga kulipiza ili
Doreen asije kumsahau.Mwalimu John alipigwa na mkewe mpaka akapoteza
fahamu ambapo mkewe alichanganyikiwa sana baada ya kumwamsha bila
mafanikio....
Endelea.....
...MWALIMU
JOHN alikuwa kimya pale kitini akiwa hana fahamu yoyote, mkewe akazidi
kuchanganyikiwa sana kwani alihisi tayari mumewe ameaga dunia.
"Jamani
mume wangu amka bado nakupenda! Nisamehe Mimi John wangu!" Alizidi
kulia mke wa mwalimu John kwa huzuni na majuto makali. Alijiona mjinga
sana kwa kujichukulia maamuzi mkononi bila hata kumdadisi vizuri.
Simanzi
ilimtanda mwanamke yule bila kujua la kufanya, machozi yalichuruzika
kama mito miwili usoni kwake kwani ndio kwanza ndoa yao ilikuwa changa
kabisa tangu waoane miezi mitano iliyopita sasa iweje John aage mapema
kiasi hicho? Mkewe aliufikiria upweke ambao angekabiliana nao Siku za
usoni. Huzuni ikamzidia.
Mwalimu John akiwa bado ameyafumba macho yake akahisi yumo kwenye usingizi mzito sana lakini alikisikia vyema kilio cha mkewe.
Alitamani
aamke ili amtulize mkewe lakini mwili ulikuwa kama umegandishwa na
sumaku. Hakuweza hata kutikisika, ghafla akahisi upepo mkali sana ndani
ya nyumba yake alipotazama ukutani akakutana na sura ya kutisha sana.
Huku
ikifuka moshi mdomoni, macho mekundu kama damu na kichwani yalichomoza
mapembe mawili marefu. John aliogogopa sana kwani tangu azaliwe hakuwahi
kukutana na kiumbe wa ajabu na wakutisha namna ile. Alitamani azinduke
usingizini lakini hakuweza, hivyo alibaki akitetemeka.
Ghafla
kiumbe yule akabadilika na kuwa sura ya msichana mrembo sana. Mwalimu
John akabaki kinywa wazi akistaajabu ya Mussa. Alipotazama vizuri
aligundua ni Doreen , akashtuka sana.Doreen alimtazama mwalimu John kwa
dharau sana kisha akaachia kicheko kikali sana.
"Mimi
ni Doreen Mbwana! Daima usinichezee maana sichezewi kirahisi.. Unataka
kuniendea Malawi we? Hahahahah umechelewa sana John, nina nguvu kuliko
unavofikiria"
Doreen
akamsogelea John, na kutoa kucha zake ndefu nyembamba kama msumari
kisha akamgusa mdomo John."Umeniita Nimekuja! Sasa utaipata fresh...!
Hahahahahahahhh" alisema Doreen kisha akatoweka . John alihema kwa nguvu
sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi kwani maneno ya Doreen
yalimtisha.
Mke
wa Mwalimu John alizidi kulia baada ya kuona mumewe haamki kwa muda
mrefu. Kelele Za kilio chake ziliwafikia majirani ambao walikuja kwa
wingi kushuhudia kilichotokea. Bila hodi majirani hao walitiririka kama
utitiri nyumbani kwa mwalimu John.
"Kuna nini jirani?" Aliuliza Mzee mmoja aliyejulikana kama Makorokocho.
"Hata sielewi mume wangu kapatwa na nini jamani...sielewi mimi" mke wa John alizidisha kilio.
"Kwani imekuaje?"
"Msogelee umwangalie maana mimi sielewi.. Namwita haamki.."
"Mh!" Aliguna Mzee Makorokocho huku akimsogelea mwalimu John.
Akamtikisatikisa John akamwita lakini John hakuitika, Ingawa John alisikia kila kitu kinachoendelea ila hakuweza kuamka.
"Mh! Mama pole sana huyu tayari ametangulia mbele za haki..."
"Ati mini?"
"Ndo ivo mama chamsingi tuwapigie ndugu zake simu, taratibu za mazishi zifanywe!"
"Hapana! Mume wangu hajafa! Iweje John afe mbele yangu.. Aaah we Mungu we!!" Mke wa Mwalimu John alilia kwa uchungu sana.
Ndugu wa mwalimu John wakapigiwa simu kupewa taarifa za msiba, taratibu za mazishi zikaanza kufanywa.
*******
Dorice
alipotoka bwenini kwao akaongoza moja kwa moja mpaka bweni la Mapambano
ambalo ndilo alilokuwa akiishi Eddy, alitembea kama mwendawazimu mpaka
alipotia timu katika bweni hill bila kujali ni bweni la wavulana pekee.
Dorice aliongoza mpaka kitanda cha Eddy ambapo alimkuta Eddy akiwa na
wenzake watatu. Na alikuwa akiwasimulia juu ya uhusiano wake mpya na
Doreen.
"Habari zenu" alisalimia Dorice akiwa amevimba kama kiboko aliyekasirishwa. Eddy hakujibu isipokuwa wale rafiki sake.
"Umefuata nini hapa we mpuuzi?"
"Nimekufuata wewe nataka nijue kama unanipenda mimi au Doreen?"
"Hivi we mwanamke unawazimu we? Nikupende wewe kama nani? Doreen ndo mpenzi wangu, nampenda sana."
"Kweli!?"
"Ndio
tena niondokee hapa, unanitia kinyaa!" Eddy alimsukuma Dorice kwanguvu
Dorice akaanguka chini na kujigongesha kichwa kwenye kitanda.
"Eddy usifanye ivo bhana utamuumiza mwenzio" alisema rafiki mmoja wa Eddy kwani alimuonea huruma sana Dorice.
"Achana nae mpumbavu huyo"
"Lakini kumbuka mlikotoka"
"Achana na mimi kama unampenda si umchukue!"
Maneno Yale yaliziidi kumuumiza Dorice, aliinuka pale chini akajifuta vumbi maana bweni lilikuwa na vumbi kupita kiasi.
"Sawa Eddy! Daima kumbuka sio kila king'aacho ni dhahabu... Utanikumbuka!" Alisema Dorice kwa huzuni na kutoka.
"Akukumbuke
nani wewe? We boya tu huna lolote" Eddy aliropoka maneno hayo huku
akiwashangaza rafiki zake kwani daima hawakujua kama Eddy angemchukia
Dorice kiasi kile kutokana na mapenzi yao yalivokuwa.
"Ama kweli watu wanabadilika..!" Alisema rafiki take Eddy na kuondoka zake.
Dorice
aliondoka zake mpaka bwenini kwao, akachukua begi lake dogo na kuweka
vitu vyake muhimu. Isipokuwa nguo za shule na madaftari, baada ya kupaki
vizuri akachukua kanga akaivaa baada ya kutoa nguo kisha akaenda bafuni
kuoga.
Alipooga
na kujiandaa vizuri alikaa kitandani kwake huku kila Mara akitazama SAA
yake ya mkononi ambayo alipewa na Eddy enzi za mapenzi yao. Ilikuwa SAA
nzuri ya Dhahabu."Ikifika SAA kumi na mbili jioni lazima nitoroke ...
Siwezi kubaki hapa!" Aliwaza Dorice akiwa kitandani kwake.
Muda
huchelewa sana pale unapousubiri ndivyo ilivokuwa kwa Dorice. Muda
ulichelewa lakini ukafika, kigiza kilipoanza tu akachukua begi lake na
kutoka bwenini. Hakuvaa nguo za shule hivyo haikuwa rahisi kugundua kama
ni mwanafunzi wa pale. Taratibu akazipiga hatua ili atoroke shuleni
pale.
Licha ya kwamba alisumbuliwa na maswali ya wanafunzi wenzake ila hakujali ingawa aliwapa majibu ya uongo yanayoridhisha.
Shule
ya mabango ilikuwa imezingirwa na miti mingi hivyo akapita katikati ya
miti hiyo ili asioneakane kirahisi. Alipokuwa anaendelea kutembea ghafla
akaona kitu mbele yake akashtuka.
********
Jioni
ile tulivu Eddy na Doreen walikutana kwenye mti mmoja mzuri na tulivu.
Walikuwa wamekumbatiana kimahaba huku wakipeana denda za kutosha.
"Baby nakupenda sana" alisema Eddy
"Nakupenda pia ila..."
"Ila nini mpenzi?"
"Sharti la kuwa na mimi ni kwamba hutuwezi kufanya mapenzi..." Alisema Doreen.
" eh! Kwanini?"
"Tukifanya hivyo kuna kitu kitatokea kwako?"
"Mh Doreen! Mbona sikuelewi, tutaishije kama wapenzi?"
"Nivumilie tu... Ila bado nina bikra"
"Nataka niitoe bikra yako Doreen please!"
" huwezi kufanya mapenzi na mimi, pia kuna sharti lingine mbali na hilo..."
"Bby hapa siwezi kuwa na wewe bila kufanya mapenzi, siwezi! Halafu pia siwezi kukuacha au huniamini?"
Alisema Eddy akiwa amezidiwa na hamu ya mapenzi na ilikuwa kazi ngumu sana kwake kujizuia....
Post a Comment Blogger Facebook