NeShante Davis akiwa na binti yake Chloe Davis-Green enzi za uhai wao. |
NeShante Davis, 26, alikutwa amefariki nyumbani kwake jirani na alipokuwa ameegesha gari lake huku binti yake aitwaye Chloe Davis-Green, akikutwa amejeruhiwa akiwa ndani ya gari la mama yake aina ya Chevrolet.
Chloe alikimbizwa hospitali ya jirani ambapo mauti yalimfika.
Majirani wa marehemu wakielezea tukio hilo walisema (juzi) Jumanne walisikia vilio vikifuatiwa na milio ya risasi kutoka nyumbani kwa Davis.
Davis, ambaye alikuwa mwalimu huko Maryland alitakiwa kuwa akilipwa Dola za Kimarekani 600 kila mwezi zikiwa ni fedha za matunzo ya mtoto katika shauri dhidi ya baba wa mtoto aitwaye Daron Boswell-Johnson.
Mwezi Desemba mwaka jana vipimo vya DNA vilionyesha kuwa Boswell-Johnson ndiye baba halisi wa mtoto Chloe na alitakiwa kumhudumia mtoto huyo.
Mtuhumiwa Boswell-Johnson alitiwa nguvuni jana (Jumatano) na kufunguliwa mashitaka ya mauaji ambayo yote alikiri kuyatenda
Post a Comment Blogger Facebook