Hatimaye Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum Act,
2015), Muswada juu ya Usimamizi wa Mafuta na Gesi, 2015 (The Oil and
Gas Revenues Management Act, 2015) na Muswada juu ya tasnia ya Uziduaji
Tanzania (The Tanzania Extractive Industries Act, 2015): The Tanzania
Extractive Industries Act, 2015
.Baadhi wa wabunge waliochangia, waliitaka serikali kuanzisha mfuko maalum wa kuwawezesha wazawa kushiriki shughuli za uchimbaji wa gesi pamoja na rasilimali nyingine zilizopo hapa nchini ili taifa liweze kunufaika nazo na kwamba mtaji usiwe kikwazo.
Akitolea ufafanuzi suala la miswada hiyo kupelekwa bungeni kwa hati ya
dharura, waziri wa katiba na sheria Mh Asharoze Migiro amesema mchakato
wa miswada hiyo ulinza siku nyingi na wadau wote walishirikishwa na wapo
baadhi ya viongozi wa halmashauri walipelekwa nje ya nchi kujifunza
hivyo kazi ya bunge ilikuwa ni kuipitia na kama kuna maboresho iboreshwe
kabla ya kusainiwa kuwa sheria.
Waziri wa Nishati na Madini Mh Simba Chawene akihitimisha mjadala huo
amesema lengo la miswada hiyo ni kuhakikisha inajenga mfumo imara wa
kisheria kusimamia sekta ya mafuta na gesi ili mwekezaji aweze kupata
stahiki yake nataifa liweze kunufaika huku akiwataka watanzania kuepuka
ushabiki wa kisiasa katika mambo ya msingi
Leo hii imepitishwa miswada miwili, Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa
Mapato ya Mafuta na Gesi wa mwaka 2015 na uwazi na uwajibikaji katika
Rasilimali za Madini Wakati Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum
Act, 2015) ulipitishwa jana Jumapili.
Miswada yote hii imepitishwa bila uwepo wa Kambi ya upinzani bungeni,
baada ya kutolewa nje na wengine kutoka wenyewe kwa kile wanachodi
kwamba Miswada yote hii imevunjwa utaratibu na kanuni za bunge katika
uwasilishaji.
Hata hivyo idadi ya wabunge wanaohudhuria vikao hivyo vya bunge ikiwemo
ya waliopitisha mswada huo imeendelea kupungua kwa kile kinachodaiwa
kuwa wengi wao wako majimboni kutokana na presha ya uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka huu.
Post a Comment Blogger Facebook