
Kikosi cha timu ya Tanzanite chini ya kocha wake mkuu Rogasian Kaijage kimeweka kambi eneo la Mbande na kufanya mazoezi yake katika uwanja wa Azam Complex kwa takribani wiki ya pili sasa kujiandaa na mchezo huo.
Msemaji wa Shirikisho la soka nchinin Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto amesema hali ya kambi ya Tanzanite ni nzuri wachezaji wote wapo katika hali nzuri na morali ya ya hali ya juu, kikubwa Watanzania wanaombwa kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi Msejai wa kuwapa sapoti timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 watakapokuwa wakicheza na wenzao wa Zambia.
Mchezo huo utachezwa siku ya jumamosi majira ya saa 10 kamili jioni katika uwanja wa Azam Complex - Chamazi, ni wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Dunia za Wanawake chini ya miaka 20 (U-20) zitakzofanyika nchini Papua New Guninea mwaka 2016.
Mwamuzi wa mchezo huo ni Batol Mahjob kutoka nchini Sudan, akisaidiwa na washika kibendera Remaz Osaman na Walaa Bilal, mwamuzi wa akiba Khadmallah Elasayed wote kutoka nchini Sudan na Kamisaa wa mchezo ni Flora Roosevelt kutoka nchini Malawi.
Post a Comment Blogger Facebook